VIJANA WA 2000 WANAONGOZA KWA UCHANGIAJI DAMU KANDA YA KATI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, June 21, 2024

VIJANA WA 2000 WANAONGOZA KWA UCHANGIAJI DAMU KANDA YA KATI.


Mkuu wa timu za ukusanyaji damu kanda ya kati Dokta Leah Kitundya amesema wanafunzi wa shule ya sekondari na vyuo wamekuwa na mwitikio mkubwa wa uchangiaji damu kwa kanda ya kati.

Makundi mengine ni Wanajeshi na wananchi wengine wenye umri kati ya miaka 18-40 ambao kati yao wanaume wanaongoza kwa kuwa na mwitikio mkubwa zaidi ikilinganishwa na wanawake.

Dokta Kitundya ameyasema hayo katika maonyesho ya Idodomia International Expo yanayoendelea katika viwanja vya Shule ya Sekondari Dodoma mkabala na bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania ambapo ametumia fursa hiyo kuwahamasisha watu kujitokeza kwa wingi kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wengine kwa kuwa licha ya mwitikio mzuri wamekuwa wakikusanya chupa za damu 1,000 kwa mwezi nje ya lengo ambalo ni chupa 1,500.

Aidha amewatoa hofu watu wanaoamini kwamba ukishatoa damu kwa mara ya kwanza ni sharti uwe na muendelezo wa kutoa damu jambo ambalo si sahihi na kwamba mtu anaweza kuendelea au kuacha na hakuna madhara yoyote yanayoweza kumpata.

Kuhusu vipindi vya kuchangia damu tangu mtu anapochangia kwa mara ya kwanza amesema kwa mwanaume ni baada ya miezi mitatu na kwa mwanamke ni miezi minne lakini mtu halazimishwi kufanya hivyo.

“Mtu anaruhusiwa kuchangia damu kila baada ya miezi mitatu kwa mwanaume na mwanamke baada ya miezi minne kwa sababu kabla ya hapo damu inakuwa haijakomaa kwa maana chembechembe hai nyekundu kwa hiyo hata ukitoa kwa wakati huo haiwezi kumsaidia mugonjwa”

Idodomia Expo imeandaliwa na Triprecy Initiative foundation, ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dodoma, Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) taasisi za mbalimbali za serikali pamoja na wadau wengine.

No comments:

Post a Comment