Polisi wa Kenya wameshutumiwa kujibu maandamano hayo kikatili |
Iwapo kuna hatua ya wazi ambayo inasubiriwa na Wakenya wengi na hasa waliokwenda barabarani kuandamana ni iwapo rais atadhihirisha kwamba alisikia kilio chao kuhusu utendakazi wa baadhi ya mawaziri wake na baadhi ya maafisa wa ngazi za juu katika utawala wa muungano wa Kenya Kwanza .
Mabadiliko katika baraza la mawaziri na pia katika uongozi wa bunge na kamati za bunge ni hatua ambayo huenda ikachukuliwa kama ufanisi kwa waandamaji waliotaka mageuzi mbali na kuukata mswada wa fedha .
Akihojiwa Jumapili iliyopita rais Ruto alipoulizwa iwapo atawafauta kazi baadhi ya mawaziri wake ambao utendakazi wao umechangia lalama za wananchi ,alijibu kwa kuashiria kwamba 'kuna jambo linalokuja' ama atachukua aina fulani ya hatua.
Wengi wanasubiri kuona kina cha hatua yake kuhusu hilo hasa baada ya wengi kulalamika kuhusu visa vya ufisadi,kiburi na kauli zinazotolewa na baadhi ya maafisa wakuu wa serikali .
Sakata kuhusu mbolea katika wizara ya Kilimo na ile ya mafuta ya kupikia katika wizara ya biashara zimetajwa kuwa baadhi ya madoa ambayo yamewakwaza wengi kwani hakuna hatua madhubuti zilizochukuliwa kwa wanaoshukiwa kuhusika .
Iwapo kuna ushirikiano ambao unaonekana kuwaghadhabisha wengi nchini Kenya ,ni ule kati ya viongozi wa kisiasa na wa kidini .
Vijana waliokuwa wakiandamana wiki mbili zilizopita walikemea vikali ushirikiano huo ambapo kwa kawaida wanasiasa nchini Kenya wamekuwa na nafasi ya wazi ya kutumia kumbi za kidini na hasa makanisa kupiga siasa,kurushiana cheche za maneno na kila aina ya matamshi ambayo hayafai kutolewa kanisani.
Kupitia kauli yao ya #Occupychurches walianza kuwazuia wanasiasa dhidi ya kuwahutubia waumini makanisani.
Ujumbe wa vijana unaonekana ulichukuliwa kwa uzito na viongozi wengi wa makanisa ambao sasa wamewapa notisi wanasiasa kwamba hali haitakuwa kama ya kawaida .
Hili ni jambo ambalo litachukuliwa kama ushindi kwa waandamanaji wa Gen Z kwani ulikuwa mtindo wa kawaida kila Jumapili kuchanganya dozi ya injili na ile ya siasa .
Kwa muda mrefu hatua hiyo iliwakera wengi na sauti za pingamizi zimekuwa wazi katika maandamano hayo .
Viongozi wa kidini pia wameshtumiwa kwa kusalia kimya wakati serikali ilipokuwa ikipendekeza sheria kali za ushuru ambazo zilionekana kuwaacha wengi katika hali mbaya kiuchumi katika mazingira ambayo tayari gharama ya maisha imewalemea wengi .
Iwapo viongozi wa kidini watataka kusalia na hadhi ya kuheshimika katika jamii,watalazimika kuchukua hatua za wazi kujitenganisha na ushirikiano wao na wanasiasa na kupaza sauti zao kupinga kinachotafsiriwa mara nyingi kama uovu wa watawala .

Polisi wa Kenya wameshutumiwa kwa kufanya ukatili walipokuwa wakiwakabili waandamanaji
Iwapo kuna kichocheo cha wazi kwa maandamano ya vijana ,ni hatua ya wanasiasa na watumishi wa serikali walio karibu na viongozi wakuu wa nchi kuonekana hadharani wakibeba na kutoa vitita vya pesa katika michango -mara nyingi katika makanisa .
Maonesho hayo ya utajiri yameashiria kutojali kwa upande wa maafisa wa serikali wanaohusika na michango hiyo.
Katika nchi ambayo wengi wana matatizo ya kichumi,mabunda ya noti machoni mwa watu ambao wanatatizika kupata hata mlo mmoja kwa siku ni chanzo cha hamaki ambayo imetokota kwa muda .
Mlipuko wa hamaki hizo ulionekana katika maandamano ya vijana wa Gen Z.
Rais William Ruto aliahidi kwamba atachukua hatua kuhusu hilo wakati alipoashiria kwamba labda wakati umewadia kwa harambee kupigwa marufuku hasa kwa maafisa wa umma .
Michango kama hiyo inashukiwa kuchochea ufisadi na inahofiwa huenda fedha za umma ndizo hutolewa katika hafla hizo.
Baadhi ya viongozi pia hawajatuliza mambo kwa kupiga picha wakiwa katika magari ya kifahari, ziara za nje ya nchi na wakistarehe katika maeneo mbalimbali ya burudani .
Iwapo maandamano ya vijana yataleta kikomo kwa 'show' hizi kubwa za ni yupi aliye na hela nyingi ,gari kubwa au jumba bora la kifahari ,basi yatakuwa yamepata ufanisi wa kuleta aina fulani ya nidhamu.

Linda Indakwa anatumia sanaa yake kuonyesha athari za maandamano katika mji mkuu. |
Iwapo kuna ushindi mkubwa ambao utaletwa na hatua ya vijana kwenda barabarani ,basi kuleta uwajibikaji kwa viongozi waliochaguliwa ndio utakaokuwa ushindi muhimu sana .
Athari za mwamko huu mpya zimeanza kuonekana.
Pingamizi ya wananchi dhidi ya mswada wa fedha ilikuwa wazi.
Wananchi walituma jumbe kwa wabunge wao,walifoka mitandaoni na kupiga kila aina ya kelele kusikika ,lakini viongozi wa kisiasa walifumbia macho malalamishi hayo na kupitisha mswada huo .
Wabunge wengi waliopiga kura ya 'Ndiyo' sasa watakuwa na kazi ya kukutana na wapiga kura.
Baadhi yao wameanza kuomba msamaha kwa wapiga kura katika maeneo bunge yao .
Iwapo watasamehewa ama adhabu ya wapiga kura ipo njiani ,ni jambo litakalosuburiwa hadi uchaguzi wa mwaka wa 2027.
Tayari chama cha upinzani cha ODM kimesema kimeanzisha mchakato wa kuwarejesha nyumbani wabunge wake sita ambao walipiga kura ya kuunga mkono mswada huo wa fedha .
Makali ya ufanisi wa maandamano kuhusu kuwaajibisha viongozi wa kisiasa kwa kweli yatakuwa wazi wakati wa uchaguzi.
Iwapo kutakuwa na athari ya kampeni ya kuwataka viongozi kuwatumikia ifaavyo wananchi ,majibu yatakuwa wazi kupitia kura kwa sababu kwa muda mrefu wanasiasa wamekuwa wakitegemea sana usahaulivu wa wapiga kura .
Wakati huu ni wazi kwamba wanakabiliana na kizazi kisichosahau na chenye ushahidi unaowachwa kote mitandaoni kuhusu 'madhila' wanayotendewa na waakilishi wao.
Swali litakuwa iwapo 'ulimama na sisi' wakati wa matatizo yetu au ulikwenda kuyashughulikia maslahi yako binafsi.
Daalili nzuri ya uwajibikaji katika matumizi ya fedha za umma ilionekana pale rais William Ruto aliposisitiza kwamba sasa kuna haja ya dharura ya Kenya kubana matumzi ya fedha za umma .
Kwanza ameashiria kwamba huenda afisi zisizo za kikatiba kama ile ya Mke wa rais na mke wa naibu wa rais zikaondolewa na mgao wa bajeti kwa afisi hizo kuelekezwa kwa matumizi mengine .
Hatua hiyo haingechukuliwa endapo vijana wa kizazi Gen Z hawangeandamana na kuzua maswali muhimu sana kuhusu matumizi ya fedha zinazolipwa kupitia kodi na wananchi .
Ingawa rais Ruto ameelezea kwa kina athari za kukataliwa kwa mswada wa fedha ikiwemo serikali kupunguza migao kwa sekta muhimu za umma,serikali za kaunti ,kukosa kuwaajiri walimu na madkatari zaidi ,amekariri pia umuhimu mkubwa uliopo wa nchi kuangalia upya jinsi inavyotumia fedha zake zinazokusanywa kama mapato ya ndani .
Alisema ni wakati mwafaka pia kuangalia kiwango cha mishahara ya maafisa wakuu wa serikali na akaeleza kuwa yuko tayari kupunguziwa mshahara katika jitihada za kuurahisisha mzigo kwa mlipa ushuru.
Kenya ingali inazongwa na madeni makubwa na itahitaji kuangalia kwa umakini matumizi yake ya fedha ili kuafikia malengo yake ya kimaendeleo .
Wataalam wa masuala ya kiuchumi wameafiki kwamba kiasi kikubwa sana cha fedha za umma hupotea kupitiia utumizi mbaya,ufujaji na ufisadi.
Mianya hii mikubwa ndio donda sugu katika utawala wowote na huenda suluhisho la kudumu lisipatikane endapo viongozi wa nchi hawataonyesha nia ya kupambana na maovu hayo kwanza kabla ya kusonga mbele .
Malalamishi ya vijana walioandamana yameifanya nchi kuanza kuyazungumzia mambo hayo .Ushahidi wa mazungumzo haya muhimu ulikuwepo siku ya Jumatano katika bunge la seneti ambapo maseneta walifungua nyoyo kuzungumzia yote haya na yanayohitaji kufanyika ili Kenya kuitumia fursa hii kama funzo na kuweza kujiweka katika mkondo ufaao wa historia .
Iwapo kuna zawadi ambayo vijana wameipa Kenya kupitia maandamano yao ,ni fursa ya kuyazungumza kwa uwazi mambo haya na kuyatafutia ufumbuzi .
No comments:
Post a Comment