Wataalam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Upanga na Mloganzila watashirikiana na wataalam wengine kutoa huduma katika Melivita ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (CPLA) kuanzia Julai 17 hadi 23, 2024 katika Kamandi ya Wanamaji (majini) Dar es Salaam.
Hayo yameelezwa leo na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa MNH, Dkt. John Rwegasha wakati akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo na kuwakaribisha Watalam waliokuja na melivita ambao wametembelea hospitalini hapo ili kukutana na wenzao watakaofanya kazi pamoja.
DKt. Rwegasha amesema MNH imejipanga kutoa watalaam wataoshiriki kutoa huduma za kibingwa katika melivita hiyo wenye kariba ya watalaam waliokuja kutoka nchini China.
Ujio wa meli hiyo unatokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya China ambao umedumu kwa kipindi kirefu.
Matibabu hayo yatatolewa bila malipo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 tangu kuasisiwa kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Septemba 1, 1964.
No comments:
Post a Comment