POLISI YAPIGA MARUFUKU KUTOA FEDHA TASLIMU WAKATI WA UKAGUZI WA VYOMBO VYA MOTO. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, July 21, 2024

POLISI YAPIGA MARUFUKU KUTOA FEDHA TASLIMU WAKATI WA UKAGUZI WA VYOMBO VYA MOTO.


Na.Mwandishi Jeshi la Polisi-Dodoma.


Jeshi la Polisi Nchini limesema kuwa Kila mwaka huadhimisha Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani huku likipiga marufuku kwa mtu yoyote kupokea ama kutoa fedha taslim wakati wa Ukaguzi wa vyombo vya moto.

Akitoa taarifa hiyo leo Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna wa Polisi DCP David Misime amesema kuwa kipindi cha kufanya ukaguzi wa vyombo vya moto wamiliki waelekezwe kurekebisha kasoro zilizobainika au kuondoa chombo husika kwa matumizi ya usafiri kama kitabainika kuwa na ubovu mkubwa.

DCP Misime ameongeza kuwa yanafanyika ni kulingana na sheria na kanuni za usalama barabarani zinavyoelekeza.

Aidha amebainisha kuwa Mwaka huu maandalizi ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani tayari yameshanza ikiwepo ukaguzi wa vyombo vya moto ulioanza toka Julai 9,2024 katika Mikoa yote.

Vilevile Ukaguzi unaofanyika kwa mwaka huu,mmiliki wa chombo cha moto atalipa ada ya ukaguzi kupitia namba ya malipo (control number) atakayopewa au atakayopakuwa kutoka katika mfumo ndipo chombo chake kitakaguliwa na kupatiwa stika.

Misime amesema kuwa Jeshi la Polisi Nchini lingependa kusisitiza katika ukaguzi unaoendelea hakuna fedha taslim itakayopokelewa mkononi ama na askari,afisa wa Polisi au wanaojifanya vishoka.Fedha yeyote kwa ajili ya ukaguzi wa chombo cha moto ilipwe kupitia mfumo wa malipo ya Serikali kwa kutumia namba ya malipo (control number).

Msemaji wa Jeshi hilo amebainisha kuwa Wamiliki wa vyombo vya moto wanasisitizwa kufuata utaratibu kwani atakayebainika kutoa malipo ya fedha ya ukaguzi wa chombo cha moto mkononi (cash) au atakayepokea malipo hayo mkononi awe mmiliki,askari,kishoka au yeyote yule atakamatwa na kufikishwa mahakamani.

No comments:

Post a Comment