Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Timu ya majadiliano ya Serikali kuhusu utekekezaji wa mkataba wa ufikishaji mawasiliano ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya Mkongo kati ya Serikali kupitia wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Kampuni ya Viettel Global Joint Stock ya Vietnam imekutana tarehe 18 Julai, 2024 ikiwa ni maandalizi ya Vikao vya majadiliano kati ya Timu ya Serikali na wawakilishi wa kutoka katika kampuni hiyo.
Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Timu ya Majadiliano ya Serikali ambaye ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Adolf Ndunguru amesema vikao hivyo ni matokeo ya vikao vya wataalam wa pande zote mbili na hatua inayofuata ni vikao vya maamuzi ili kuhitimisha majadiliano hayo.
“Tumekutana leo hapa kufungua tena majadiliano upya na kampuni ya Viettel, majadiliano haya tulianza mwaka 2021 katika mgogoro wetu wa uwekezaji wa mkongo kwenye maeneo mbalimbali, leo tumekutana timu ya wataalam wa ndani na kamati ya majadiliano ya kitaifa, kesho tutakutana na wenzetu wa Viettel ili kupeana fursa za kupata mawasiliano mazuri na kuhitimisha mgogoro huo ili tulete maendeleo kwa Wananchi na hatimaye tupekele mawasiliano bora vijijini” amesema Bw. Ndunguru.
No comments:
Post a Comment