TRC YAOMBA RADHI KWA HITILAFU YA UMEME ILIYOSIMAMISHA TRENI KWA SAA MBILI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, July 31, 2024

TRC YAOMBA RADHI KWA HITILAFU YA UMEME ILIYOSIMAMISHA TRENI KWA SAA MBILI


Dar es Salaam, Tarehe 31 Julai 2024


Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeomba radhi kufuatia hitilafu ya umeme iliyojitokeza kati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete na kusababisha treni ya reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) iliyokuwa inasafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma kusimama kwa muda wa saa mbili (2) siku ya tarehe 30 Julai 2024.

Kwa mujibu wa Taarifa za awali zilizotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano TRC Jamila Mbarouk zinaonesha kuwa hitilafu za aina hiyo husababishwa na wanyama (ngedere) au ndege (bundi) wanapogusa nyaya za umeme zilizotandazwa juu ya reli (overhead catenary system). Hitilafu ilisababisha umeme kukatika kituo cha kupoozea umeme namba 7 (Godegode) ambayo kitaalamu hujulikana kama (Instanteneous Overcurrent Protection Trip) majira ya saa 4:20 usiku.

"Mafundi wa TRC walifanikiwa kutatua changamoto na kurejesha umeme saa 6:30 usiku na treni kuendelea na safari kuelekea Dodoma, na kuwasili Dodoma majira ya saa 7:57 usiku"

Shirika la Reli Tanzania linaomba radhi kwa usumbufu uliotokea.

No comments:

Post a Comment