🎈🎈TANESCO kuunganisha mkoa wa Katavi kwenye Gridi ya Taifa Septemba 2024
🎈🎈Bilioni 2.2, bili ya Dizeli ya Majenereta kila mwezi kuokolewa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Julai 13,2024 amefanya ukaguzi wa kituo cha kupokea kupoza na kusafirisha Umeme cha Inyonga, wilayani Mlele, mkoani Katavi na kujionea maendeleo ya Mradi huo ambao umekamilika kwa asilimia 97.
Mhe.Dkt Samia amesema kuwa mara baada ya kukamilika kwa Mradi huo Septemba 2024,Mkoa wa Katavi utaingizwa rasmi kwenye Gridi ya Taifa na hivyo kuachana na uzalishaji wa umeme kwa majenereta yanayozalisha Umeme kwa mafuta ya Dizeli.
"Tunakwenda kuzima majenereta ya mafuta, tunakwenda kuiweka Katavi katika Gridi ya Taifa,na tutaokoa shilingi Bilioni 2.2 za kununua mafuta kila mwezi"
Dkt Samia amesema kuwa Serikali imetumia kiasi cha Shilingi Bilioni 164,ambapo inahusisha ujenzi wa vituo vya kusafirisha na kupoza Umeme cha Ipole,Inyonga na Mpanda pamoja na ujenzi.
No comments:
Post a Comment