UMAHIRI WA MAAFISA WAWAKOSHA VIONGOZI WALIOTEMBELEA BANDA LA WIZARA YA FEDHA-SABASABA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, July 12, 2024

UMAHIRI WA MAAFISA WAWAKOSHA VIONGOZI WALIOTEMBELEA BANDA LA WIZARA YA FEDHA-SABASABA


Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Bw. Godfred Mbanyi, akizungumza na Afisa Habari Mwandamizi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Ramadhani Kissimba (kushoto), kuhusu umuhimu wa elimu kwa umma ili kuchochea maendeleo, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katıka Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Bw. Fransis Mwakapalila, akipongeza umahiri wa watoa huduma katika Banda la Wizara ya Fedha alipotembelea Banda hilo katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari Mwandamizi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Ramadhani Kissimba.

Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Hozen Mayaya (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Chuo hicho alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katıka Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Bw. Godfred Mbanyi, akipakua taarifa za Filamu kuhusu elimu ya Fedha, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katıka Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam, ambapo njia hiyo inarahisisha kuifikia filamu hiyo kwa njia ya simu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Bw. Godfred Mbanyi, akipakua taarifa za Filamu kuhusu elimu ya Fedha, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katıka Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam, ambapo njia hiyo inarahisisha kuifikia filamu hiyo kwa njia ya simu.

Afisa Kumbukumbu wa Kitengo cha Pensheni Wizara ya Fedha, Bi. Neema Nyipamato akitoa maelezo ya majukumu ya Ofisi ya Pensheni-Hazina, kwa Mzee Amosi Gakutwa, kuwa ni pamoja na kulipa mafao kwa viongozi wa kitaifa na kisiasa na watumishi wa umma ambao hawachangii katika mifuko ya hifadhi ya jamii, wakati wa Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Bw. Godfred Mbanyi, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katıka Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam, ambapo amesisitiza umuhimu wa elimu kwa umma ili kuchochea maendeleo.

Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Bi. Janeth Hiza, akitoa elimu ya fedha kuhusu uwekaji wa akiba, uwekezaji na mikopo kwa vijana waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.

Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Bi. Janeth Hiza (wa tano kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na maafisa kutoka Wizara hiyo, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)


Na. Peter Haule, WF, Dar es Salaam


Viongozi mbalimbali waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam, wameipongeza Wizara ya Fedha kwa kuwa na mikakati mizuri ya utoaji wa elimu kwa umma kuhusu Majukumu na Sera za Wizara Fedha, ili kuchochea maendeleo.

Baadhi ya viongozi waliotembelea Banda ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Bw. Godfred Mbanyi, Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Hozen Mayaya, Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Bw. Fransis Mwakapalila na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha wa Wizara ya Fedha, Bi. Janeth Hiza.

No comments:

Post a Comment