Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu Balozi Nchimbi ameambatana na Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Ndugu Issa Haji Usi Gavu, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa - Oganaizesheni, Ndugu Amos Gabriel Makalla, Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo na Ndugu Rabia Hamid Abdalla, Katibu wa NEC - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.
Malengo ya ziara hiyo ya Katibu Mkuu wa CCM ni pamoja na kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2020 - 2024, kukagua na kuhamasisha uhai wa CCM, pamoja na kuzungumza na kuwasikiliza wananchi.
No comments:
Post a Comment