Ashrack Miraji Same Kilimanjaro
Wanachama wa ushirika wametoa shukran za dhati Kwa mdau huyo kushiriki zoezi la ujenzi wa mfereji ambao unaohudumia zaidi ya kaya 500 kata ya Makuyuni wilaya ya Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro, Mfereji huo wa maji walikuwa wanautumia Kwa shughuli Mbalimbali za kijamii kama kilimo cha mboga mboga na kunyweshwea mifugo
Akizungumza Kwa njia ya simu na kituo hiki koola alisema wanachama walijikuta katika wakati mgumu baada ya birika linalovusha maji kuharibika vibaya na kushindwa kuvusha maji kwenda kwenye mfereji huo na kuleta changamoto hiyo ambayo imejitokeza kwa Mara ya pili sasa.
Viongozi hao waliitaarifu bodi ya tume ya umwagiliaji walifika na kuangalia adhari hizo na kutoa ushauri ukarabati mkubwa ufanyike kwa dharura ili wananchi waendelee kupata huduma ya Maji ya kumwagilia na kunyweshea mifugo yao.
Sambamba na hayo yote baadhi ya viongozi wa mfereji huo wakiongozwa na Jafar mfinanga waliitisha mkutano wa watumiaji wa Mfereji huo na Wadau Mbalimbali lengo kuweza kusaidiwa kukarabati miundombinu ya mfereji huo kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa haraka ,
" Tuliwasiliana na Mhe. Naibu Waziri Ummy ambaye ni mzaliwa wa Makuyuni na aliahidi kutuchangia laki 2, pamoja na Mhe. Diwani akatuchangia sh laki 1 na nusu, Mama Santorin akatuchangia sh laki 2.
Na kuongeza kuwa, “Pia tulimpigia mdau wa maendeleo ndugu Enock Koola na kwa haraka alikubali kushirikiana na wananchi wa kata ya Makuyuni kwa kuchangia sh laki tano na kuahidi atashirikiana nasi zaidi endapo tukikwama Kwa mara nyingine, amesema Mfinanga."
No comments:
Post a Comment