MAFUNZO YA UHAKIKI MFUMO WA ANWANI ZA MAKAZI YAFUNGULIWA PEMBA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, August 1, 2024

MAFUNZO YA UHAKIKI MFUMO WA ANWANI ZA MAKAZI YAFUNGULIWA PEMBA


Afisa Mdhamini kutoka Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar anayeshughulikia eneo la Pemba Bw. Ibrahim Saleh Juma, amefungua mafunzo kwa Masheha na Makatibu wa Masheha kuhusu zoezi la uhakiki wa taarifa za anwani za makazi katika Wilaya za Wete na Mkoani zilizopo Pemba, Zanzibar.
Akifungua mafunzo hayo tarehe 01 Agosti, 2024 Bw. Ibrahim amesema “Lengo la mafunzo hayo ni kujenga uwezo kwa Masheha na Makatibu wao ili waweze kutekeleza vyema zoezi la kuhakiki taarifa za Anwani za Makazi ikizingatiwa kuwa zoezi hilo ni endelevu”.
Ameongeza kuwa hatua hiyo itawezesha upatikanaji wa taarifa sahihi za ukaazi na hivyo kujenga mazingira bora ya utoaji na ufikishaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi.


Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Posta kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bi. Caroline Kanuti amesema kuwa utekelezaji endelevu wa Mfumo wa Anwani za Makazi unahitaji juhudi za pamoja miongoni mwa wadau.

Aidha ametoa rai kwa wataalam na waratibu kuandaa mipango na mikakati ya kuhakikisha utekelezaji wa Mfumo huo unafanyika katika mazingira endelevu.


Miongoni mwa waliohudhuria mafunzo hayo ni Mratibu wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali Bw. Bakari Mwamgugu ambapo kupitia mradi huo unaotekelezwa chini ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, mradi wa mfumo wa Anwani za Makazi ni moja ya eneo linalofadhiliwa na mradi huo.

No comments:

Post a Comment