CHUO kikuu cha Ardhi kimeanzisha mfumo wa shamba bot utakaotumia akili bandia lengo likiwa ni kusaidia wakulima waweze kulima kisasa.
Akizungumza katika maonesho ya nanenane jijini Dodoma leo Agost 6, 2024 Muhitimu wa Chuo hicho na mbunifu wa mfumo huo wa Shamba Bot Godfrey Enishi amesema, kuwa chuo hicho kimeanzisha mfumo huo wa shamba bot ili kumrahisishia kazi mkulima.
"Mfumo huo wa Shamba Bot ndio afisa ugani, a utakuwa unampa mkulima taarifa mbalimbali kuhusiana na kilimo na pia mfumo huo utatoa ushauri wa namna ya kulima,
Kutokana na maafisa ugani Tanzania kuwa wachache ndio maana tumekuja na huu mfumo kwasababu maafisa ugani Tanzania wapo takribani elfu saba na ukiangalia idadi ya wakulima ni wengi sana dhidi ya maafisa"amesema
Amesema kuwa mfumo huo utamuelekeza mkulima ni aina gani ya kilimo anapaswa kulima kutokana na jografia ya eneo husika.
Aidha amesema kuwa mfumo huo ni mpya kwani umeanza rasmi Januari mwaka huu lakini umeleta matokeo chanya kwa wakulima
"Mpaka sasa hivi tunaendelea na zoezi la kuupa mfumo huo data nyingi ili uweze kuwa unatoa majibu sahihi, mpaka sasa hivi tumefikia asilimia 85 na nimaendeleo mazuri kwa mfumo "amesema
No comments:
Post a Comment