Tarehe 23 Agosti 2024, Mhe. Phaustine Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji alikutana na Ujumbe wa Tanzania unaoshiriki Vikao vya Ngazi Wataalamu kuhusu Soko Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) vilivyofanyika Jijini Maputo, Msumbiji kuanzia tarehe 19 hadi 23 Agosti, 2024.
Ujumbe huo ulifika kwenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania ziliopo Maputo kwa ajili ya kumsalimia Mhe. Balozi pamoja na kumueleza majadiliano yanayoendelea ndani ya AfCFTA na hatua zilizofikiwa katika Vikao vyao vya Wataalamu ambavyo vinahusisha; Kamati ya Biashara ya Kidijitali, Kamati ya Utatuzi wa Migogoro ya Kibiashara na Kamati ya Wanawake na Vijana katika Biashara ndani ya AfCFTA.
Vikao hivyo, vitafuatiwa na Mkutano wa Ngazi ya Makatibu Wakuu wa Nchi zilizozosaini Mkataba wa AfCFTA utakaofanyika tarehe 26 hadi 29 Agosti 2024, jijini Maputo.
Imetolewa na Ubalozi wa Tanzania - Msumbiji
23 Agosti, 2024
No comments:
Post a Comment