Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Zainab Katimba amesema Serikali itaendelea kufanya matengenezo ya barabara katika Zahanati ya Mawela ili kurahisisha utoaji huduma kwa Wananchi wa Moshi Vijijini kama ilivyokusudiwa.
Mhe. Katimba amesema hayo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mheshimiwa Felista Deogratius Njau, aliyeuliza Je, ni lini Serikali itajenga barabara ya kutoka Kisomboko kwenda Zahanati ya Mawela, Moshi Vijijini kwa kiwango cha changarawe?
Amesema inakadiriwa kuwa na Kilomita 3 ya barabara hiyo ambayo haijasajiliwa katika mtandao wa barabara zinazohudumiwa na Tarura, barabara hiyo ni moja kati ya barabara zinazoelekea Zahanati ya Mawela ikiwa ni pamoja na barabara ya Uru Seminari, Kifunguni ambayo ni Kilomita 4.5 na Murangi, Kisalika High School ambayo ni Kilomita 3 ambayo kwa mwaka 2024/2025 itafanyiwa matengenezo ya kawaida kwa gharama ya Shilingi Milioni 900.
Mhe. Katimba amesema mwaka 2024/2025 Ofisi ya Rais Tamisemi kwa kushirikiana na Wananchi wa maeneo husika itahakikisha barabara ya Kisomboko, Zahanati ya Mawela inafanyiwa matengenezo ili iweze kupitika na kutoa huduma.
Aidha Mhe. Katimba amesema katika mwaka wa fedha 2024/2025 barabara ya Mawela Kanisani kwenda Zahanati ya Mawela itafanyiwa matengenezo ili iweze kupitika na kutoa huduma iliyokusudiwa kwa Wananchi.
“Tayari vikao hivyo vimeshaketi tarehe 13, Novemba 2023 kikao cha bodi ya barabara ya Mkoa ilikaa na kupitisha barabara zenye urefu wa Kilomita 413 ni maombi ya kwa ajili ya kupitishwa ili yaweze kuingia katika mtandao utakao hudumiwa na Tarura, Serikali inachukua hatua barabara hizi tayari zimeshapitishwa kwenye utaratibu bado kudhibitishwa ili zianze kuhudumiwa na Tarura" Mhe. Katimba
No comments:
Post a Comment