TFRA YATAKIWA KUTOA ELIMU YA MATUMIZI YA MBOLEA KATIKA MAZAO YA BIASHARA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, August 4, 2024

TFRA YATAKIWA KUTOA ELIMU YA MATUMIZI YA MBOLEA KATIKA MAZAO YA BIASHARA



Na Renatha Msungu MWANZA


MWENYEKITI wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini (TFRA) , Antony Dialo amewataka mamlaka hiyo kutoa elimu ya matumizi ya mbolea kwenye mazao ya biashara kama Pamba.

Amesema Pamba ni zao kubwa la biashara na mikoa ya Kanda ya Ziwa wanalima kwa wingi hivyo ni vyema wakapewa elimu hiyo.

Amefafanua kuwa wakulima wakilima zao la Pamba kwa kutumia mbolea watavuna pamba nyingi ambayo itawainua kiuchumi.

Anasema TFRA inapaswa kuliangalia hilo,ili wakulime wajue umuhimu wa kutumia mbolea mbali mbali kwenye kilimo.

Kwa upande wake Meneja TFRA Kanda ya Ziwa Michael Sanga amesema kwa sasa mamlaka hiyo iko katika kampeni za wakulima kutumia mbolea.

Amesema hivi sasa wakulima wengi wameanza kupata elimu ya matumizi sahihi ya mbolea kwa ajili ya msimu wa kilimo.

No comments:

Post a Comment