UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2024 KUFANYIKA NOVEMBA 27 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, August 15, 2024

UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2024 KUFANYIKA NOVEMBA 27





Na Okuly Julius, Dodoma


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohammed Mchengerwa, amesema uchaguzi wa serikali za mitaa Tanzania Bara kwa mwaka 2024 utafanyika Novemba 27 na Upigaji wa kura utaanza
saa mbili kamili asubuhi na kumalizika saa kumi kamili jioni.

Waziri Mchengerwa ameyasema hayo leo Agosti 15,2024 Jijini Dodoma , wakati akitoa tangazo la uchaguzi wa serikali za Mitaa kwa mwaka 2024 lililoambatana na uzinduzi wa nembo itakayatumika kwenye uchaguzi pamoja na utolewaji wa muongozo wa uchaguzi huo.

"Nafasi zitakazogombewa katika uchaguzi huu
ni Mwenyekiti wa kijiji, wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (kundi mchanganyiko la wanaume na wanawake), wajumbe wa Halmashauri
ya Kijiji (kundi la wanawake) na wenyeviti wa vitongoji katika Mamlaka
za Wilaya.Kwa nafasi hizo,uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa
Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri
ya Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Wilaya za Mwaka
2024 (Tangazo la Serikali Na. 571 la Mwaka 2024), nyingine ni Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji Midogo. Kwa nafasi
hiyo, uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji Midogo za Mwaka
2024 (Tangazo la Serikali Na. 572 la Mwaka 2024),

Nakuongeza kuwa "nafasi nyingine ni Mwenyekiti wa kijiji, wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (kundi
mchanganyiko la wanaume na wanawake), wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (kundi la wanawake) na wenyeviti wa vitongoji katika Mamlaka
za Miji. Kwa nafasi hizo, uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa
Halmashauri ya Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za
Miji za Mwaka 2024 (Tangazo la Serikali Na.573 la Mwaka 2024) na Mwenyekiti wa mtaa na wajumbe wa kamati ya mtaa (Kundi
Mchanganyiko la Wanaume na Wanawake) na wajumbe wa kamati ya
mtaa (Kundi la Wanawake) katika Mamlaka za Miji. Kwa nafasi hizo,
uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa
Mwenyekiti wa Mtaa na Wajumbe wa Kamati ya Mtaa katika Mamlaka
za Miji za Mwaka 2024 (Tangazo la Serikali Na. 574 la Mwaka 2024), " ameeleza Mchengerwa

Aidha, katika hatua nyingine Mchengerwa amezitaka Taasisi zinazotaka kutoa elimu ya mpiga kura kufanya maombi maalumu kupitia kwa Katibu Mkuu wa ofisi ya Rais TAMISEMI ili wapate kibali cha kutoa elimu hiyo kwa kuzingatia miongozo iliyotolewa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Ndg. Juma Ali Khatibu amesema wao kama Baraza la Vyama vya Siasa hawategemei kuona migogoro baada ya Uchaguzi kwani kuna maisha mengine yataendelea baada ya Uchaguzi.

Pia ametoa wito kwa watendaji wa TAMISEMI watakaohusika katika usimamizi wa mchakato wa uchaguzi huo kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa haki na weledi na kuzingatia Taaluma zao na misingi ya Haki ili kutimiza zile 4R za Rais Samia.

Naye Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa Martin Shigella amesema ushiriki wa Viongozi wa vyama vya siasa katika mchakato wa leo unakwenda kuongeza hari na hamasa kwa wananchi kushiriki katika uchaguzi huo.

"Hata sisi kule mikoani tuna viongozi wa vyama vya siasa na tunashirikiana nao Sana katika kuhakikisha uchaguzi huu una kuwa wa haki na uhuru ili kuhakikisha wanapatikana viongozi bora ambao watatanguliza maslahi ya Taifa mbele," ameeleza Shigella

Kampeni za UCHAGUZI wa serikali za mitaa 2024 zitafanyika siku saba
kabla ya siku ya uchaguzi. Aidha, Kanuni zinaelekeza, kila Chama cha
Siasa kinachoshiriki uchaguzi kitawasilisha ratiba yake ya mikutano ya
kampeni ya uchaguzi kwa Msimamizi wa Uchaguzi si chini ya siku saba
kabla ya kuanza kwa kampeni.






No comments:

Post a Comment