Na Okuly Julius Dodoma
KATIBU Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka amezitaka Wizara na Taasisi za Umma kuhakikisha wanatenga Bajeti na kuweka Programu ya michezo katika maeneo yao ya kazi kwani michezo ni muhimu kama shughuli zingine zozote.
Kusiluka ametoa kauli hiyo leo Agosti 10,2024 jijini Dodoma, wakati akizungumza katika Bonanza la Shirikisho la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI),ambapo amesema siku moja haitoshi kwa michezo hivyo ni vyema kila Idara iandae programu za michezo na ataanza kuzifuatilia.
"Mimi mwenyewe nafanya mazoezi na ofisini pale tuna eneo maalumu la kufanyia mazoezi hivyo nizitake Wizara na Idara za Serikali kuwa na Programu za mazoezi," amesema Balozi Kusiluka
Pia amewataka viongozi wote kuanzia Makatibu Wakuu kuhakikisha wanampatia taarifa ya namna gani wameandaa Bajeti kwa ajilili ya michezo na kutokuwa na Bajeti isiwe kikwazo kwa watumishi kutoshiriki katika Michezo.
Pia amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Gerson Msigwa kuhakikisha wananchi na watumishi wa Umma wanahamasishwa kushiriki michezo kwani sio kila michezo inahitaji Bajeti kubwa nyingine ni hamasa tu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa SHIMIWI, Daniel Mwalusamba amesema kuwa Mashindano ya SHIMIWI kwa mwaka 2024 yatafanyika Mkoani Morogoro Kuanzia Septemba 18 hadi Oktoba 5 hivyo kuwaomba waajiri kuwaruhusu Mapema watumishi wao ambao ni wanamichezo ili kushiriki michezo hiyo na kusaidia kuanza kwa wakati bila kuathiri ratiba za Mashindano.
"Kufuatana na Kumbukumbu tulizonazo baadhi ya Timu huwa zinachelewa kufika katika mashindano hali inayopelekea kuvurugika kwa ratiba hivyo tuwaombe waajiri kuwaruhusu Mapema wanamichezo kuja kushiriki mashindano ya SHIMIWI kwa wakati ili kuepukana na mvurugiko wa ratiba,"ameeleza Mwalusamba
Amesema lengo Kuu la Mashindano ya SHIMIWI ni kuhakikisha watumishi wa umma wanakuwa na Afya njema ili waweze kutoa mchango wa ujenzi endelevu wa Taifa hivyo michezo ni eneo salama la kutunza afya za Watumishi.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Gerson Msigwa amesema Wizara hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Afya ina kampeni ya kupinga magonjwa yasiyoambukiza kupitia michezo na kampeni hiyo itasaidia Watanzania wote waanze kufanya mazoezi.
"Kwa sasa kila mahali kuna Jogging ni kuonesha kuwa watanzania wanaunga mkono michezo na kupinga magonjwa yasiyoambukiza kupitia michezo na kutakuwepo na afua mbalimbali za kuhakikisha kampeni hii inafanikiwa kwani tayari tumeshafanya mazungumzo na Wizara ya Mambo ya Ndani maana wenzetu wana vikosi vya Polisi nchi nzima na Wizara ya Ulinzi nao wana Vikosi nchi nzima hivyo wenzetu watatusaidia kuhamasisha mazoezi sio kwa Wafanyakazi tu ila hata kwa wanachi, " amesema Msigwa

No comments:
Post a Comment