WIZARA YA FEDHA YATOA MAFUNZO MFUMO WA UANDAAJI NA USIMAMIZI WA BAJETI (CBMS) - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, August 14, 2024

WIZARA YA FEDHA YATOA MAFUNZO MFUMO WA UANDAAJI NA USIMAMIZI WA BAJETI (CBMS)

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akifungua Kikao kazi cha mafunzo ya Mfumo wa Uandaaji na Usimamizi wa Bajeti (CBMS) ulioboreshwa, ambacho kitaambatana na kufanya tathmini ya utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2023/2024 ili kuweka mikakati itakayosaidia kuboresha uandaaji wa mipango na bajeti kwa mwaka 2025/2026, jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa kuhusu Mfumo wa Uandaaji na Usimamizi wa Bajeti (CBMS) ulioboreshwa, wakati wa Kikao kazi kilichowashirikisha wataalamu kutoka Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali na Sekretarieti za Mikoa, jijini Dodoma.
Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Bajeti Wizara ya Fedha, Bw. Fundi Makama (kushoto) na Raymond Khohelera, wakifuatilia mada wakati wa ufunguzi wa Kikao kazi cha mafunzo ya Mfumo wa Uandaaji na Usimamizi wa Bajeti (CBMS) ulioboreshwa, ambacho kimewashirikisha wataalamu kutoka Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali na Sekretarieti za Mikoa, jijini Dodoma.
Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Fred Mdolo (kulia) na Mchumi kutoka Mkoa huo Bw. Shipembe Tanganyika, wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa kuhusu Mfumo wa Uandaaji na Usimamizi wa Bajeti (CBMS) ulioboreshwa, wakati wa Kikao kazi kilichowashirikisha wataalamu kutoka Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali na Sekretarieti za Mikoa, jijini Dodoma.
Washiriki wa Kikao kazi cha mafunzo ya Mfumo wa Uandaaji na Usimamizi wa Bajeti (CBMS) ulioboreshwa wakifuatilia mafunzo hayo ambayo yatasaidia kuboresha uandaaji wa mipango na bajeti kwa mwaka 2025/2026, Kikao kazi hicho kimewashirikisha wataalamu kutoka Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali na Sekretarieti za Mikoa, jijini Dodoma, jijini Dodoma.
Baadhi ya Maafisa kutoka Idara ya Usimamizi wa Bajeti Wizara ya Fedha, wakiwa katika Kikao kazi cha mafunzo ya Mfumo wa Uandaaji na Usimamizi wa Bajeti (CBMS) ulioboreshwa ambacho kimeshirikisha wataalamu kutoka Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali na Sekretarieti za Mikoa, jijini Dodoma.



(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)

Na. Peter Haule, WF. Dodoma

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, amefungua Kikao kazi cha mafunzo ya Mfumo wa Uandaaji na Usimamizi wa Bajeti (CBMS) ulioboreshwa ambacho kitaambatana na kufanya tathmini ya utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2023/2024 ili kuweka mikakati itakayosaidia kuboresha uandaaji wa mipango na bajeti kwa mwaka 2025/2026.

Akizungumza jijini Dodoma kwa niaba ya Katibu Mkuu Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, alisema kuwa lengo la kikao hicho ni kupata mafunzo ya Mfumo wa CBMS ulioboreshwa na kujadili kuhusu mafanikio na changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2023/2024 ili kubaini maeneo ya kuboresha.

Alisema kuwa Kikao kazi hicho kimegawanywa katika makundi mawili ambapo kundi la kwanza limeanza mafunzo na kundi la pili linatarajiwa kuanza mafunzo Agosti 21, 2024.

Bi. Omolo alisema kuwa ushiriki wa wajumbe katika Kikao kazi hicho utasaidia kuboresha utekelezaji na usimamizi wa bajeti ya Serikali, kuongeza ufanisi katika mchakato wa bajeti na kuhakikisha vipaumbele vya Serikali vinatekelezwa ipasavyo.

Vilevile aliwataka washiriki wa kikao kazi hicho kushiriki kikamilifu katika mafunzo na kuuliza maswali yatakayowezesha kuuelewa vizuri na kuutumia Mfumo huo wa CBMS ili kuimarisha utekelezaji na usimamizi wa bajeti ya Serikali

Aidha, aliwafahamisha washiriki wa mafunzo kuwa mchakato wa maandalizi ya Mwongozo wa Mpango na Bajeti ya Mwaka 2025/2026 umeanza, hivyo ushauri na mapendekezo yatakayotokana na kikao kazi hicho yatasaidia katika kuboresha maandalizi ya Mwongozo huo.

Wizara ya Fedha katika kusimamia maandalizi na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali, inafanya mafunzo ya Mfumo wa Uandaaji na Usimamizi wa Bajeti (CBMS) ulioboreshwa uliounganishwa na Mfumo wa Ulipaji Serikalini (MUSE) ili kurahisisha uingizaji wa takwimu za bajeti.

Kikao kazi kimeshirikisha wataalamu kutoka Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali na Sekretarieti za Mikoa.

No comments:

Post a Comment