BILIONEA MULOKOZI AJITOKEZA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA . - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, September 7, 2024

BILIONEA MULOKOZI AJITOKEZA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA .


Na Mwandishi Wetu,Manyara .

Bilionea Mulokozi ambaye pia Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kuzalisha vinywaji changamshi ya Mati Super Brands Limited David Mulokozi amejitokeza kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la Wapiga kura katika kituo Cha Bagara Sekondari Wilayani Babati Mkoani Manyara huku akieleza kufurahishwa na zoezi hilo linaloendeshwa kwa ufanisi mkubwa na Tume Huru ya Uchaguzi na kuwataka wakazi wa Mkoa huo kujitokeza kwa wingi.


Mulokozi amesema kuwa zoezi hilo linafanyika kwa utaratibu mzuri ambao unamuwezesha kila mwananchi kujiandikisha na kuendelea na shughuli za uzalishaji mali bila kuathiri ratiba zao za kila siku.

“Mimi leo nimetimiza haki yangu ya kujiandikisha ili niweze kushiriki Uchaguzi wa Serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu 2025 na imechukua dakika chache kwasababu nilishawahi jiandikisha hivyo nilikua nahamisha taarifa zangu kuja hapa ninapoishi sasa hivi” Anaeleza Mulokozi.

Mulokozi amewataka vijana na wakazi wa mkoa huo kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kujindikisha kwani zoezi hilo halichukui muda na hakuna foleni.

No comments:

Post a Comment