CHALINZE YAFIKIWA NA ELIMU YA FEDHA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, September 5, 2024

CHALINZE YAFIKIWA NA ELIMU YA FEDHA


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Bw. Ramadhani Possi, (wa pili kulia), akizungumza na timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha waliofika kwa lengo la kutoa elimu ya fedha kwa wananchi ili kuwawezesha kuepukana na mikopo umiza pamoja na kujifunza kuhusu riba, mikopo, dhamana pamoja na uwekezaji, ofisini kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze.

Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Wizara ya Fedha Bw. Stanley Kibakaya, akitoa elimu ya fedha kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutumia taasisi za fedha zilizosajiliwa wanapochukua mikopo ili kuwawezesha kuondokana na mikopo umiza pamoja na umuhimu wa kuzingatia mapato na matumizi ili wajiwekee akiba, wakati Maafisa wa Wizara ya Fedha walipokuwa wakitoa elimu ya fedha kwa wananchi katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Chalinze.

Afisa Usimamizi wa Fedha Mwandamizi wa Wizara ya Fedha, Bi. Mary Mihigo, (mwenye sare), akifafanua jambo kwa wananchi mara baada ya kukamilika kwa programu ya elimu ya fedha kwa wananchi inayotekelezwa na Wizara ya Fedha, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Chalinze.

Afisa Masoko na Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Uwekezaji wa UTT AMIS, Bw. Rahim Mwanga, akiwaelekeza wananchi kuhusu mifuko ya uwekezaji inayopatikana katika Mfuko wa Uwekezaji wa UTT Amis na jinsi wanavyoweza kunufaika na fursa za uwekezaji, wakati wa mafunzo ya elimu ya fedha iliyotolewa na Maafisa kutoka Wizara ya Fedha, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Chalinze.

Afisa Maendeleo Mwandamizi Halmashauri ya Chalinze, Bw. Ramadhani Mtumba, akitoa ufafanuzi kwa wananchi waliohudhuria katika programu ya utoaji wa elimu ya fedha kwa wananchi inayotekelezwa na Wizara ya Fedha, kuhusu mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na Serikali, taratibu za kufuata ili kupata mikopo hiyo pamoja na jinsi ya kusajili vikundi na namna ya kuwawezesha kupata fursa ya mikopo husika, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Chalinze.

Afisa Masoko na Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Uwekezaji wa UTT AMIS, Bw. Rahim Mwanga, akiwaelekeza wananchi jinsi ya kufungua akaunti za uwekezaji katika Mfuko wa Uwekezaji wa UTT Amis kwa kutumia simu za mkononi, baada ya kukamilika kwa mafunzo ya elimu ya fedha iliyotolewa na Maafisa kutoka Wizara ya Fedha, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Chalinze.

Baadhi ya wananchi wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa na Maafisa kutoka Wizara ya Fedha waliowasili kutoa elimu ya fedha kwa wananchi, kuhusiana na usimamizi wa fedha binafsi, dhamana za mikopo, riba pamoja na uwekezaji, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Chalinze.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Chalinze -Pwani)


Na. Saidina Msangi, WF, Chalinze


Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha, imefika Halmashauri ya Chalinze Mkoani Pwani kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha kwa wananchi itakayo wawezesha kuepukana na mikopo umiza pamoja na kujifunza kuhusu riba, mikopo, dhamana na uwekezaji.

No comments:

Post a Comment