Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini Naibu Kamishna wa Polisi DCP Ramadhan Ng’anzi amefika Jijini Arusha na kufanya ukaguzi wa kushtukiza wa vyombo vya moto na kutoa onyo kwa baadhi ya madereva wanaotumia vilevi wakati wa kuendesha vyombo hivyo.
DCP Ng’anzi amebainisha hayo katika eneo la kisongo Jijini Arusha ambapo amebainisha kuwa katika kikao kilicho fanyika hivi karibu Shule ya Polisi Tanzania Mjini Moshi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alilitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha wanadhibiti ajali hapa Nchini.
Aidha amesema kuwa operesheni hiyo ni endelevu na inafanyika nchi nzima huku akiwaomba abiria kutoshabikia mwendo kasi na badala yake watoe taarifa kwa Jeshi hilo ili madereva wezembe wachukuliwe hatua.
No comments:
Post a Comment