Na. Lusungu Helela -Morogoro
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Deus Sangu amekutana na kufanya mazungumzo na wachezaji wa michezo mbalimbali wanaoshiriki SHIMIWI kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambapo amewataka Wachezaji hao kuhakikisha wanarudi na ushindi
Naibu Waziri Mhe.Sangu ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja tangu Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe.Doto Biteko kufungua mshindano ya 38 ya SHIMIWI yanayoendelea Kitaifa Mkoani Morogoro
Mbali na ushindi, Mhe.Sangu amewataka Wachezaji hao kuyatumia mashindano hayo kuimarisha mahusiano baina yao pamoja na kujenga afya ili pindi watakaporudi katika maeneo yao ya kazi wakaongeze ufanisi katika kuwahudumia wananchi.
Amesema Mashindano ya aina hiyo mbali na kuwauganisha watumishi, lakini yanawezesha mshikamano miongoni mwao na kujenga afya ambayo ndio msingi wa utendaji bora wa kazi na wenye tija
Amesema anatambua kuwa mashindano hayo yana ushindani mkubwa lakini kutokana na maandalizi ambayo Ofisi yake wameyafanya ushindi ni jambo la lazima
Katika hatua nyingine, Mhe.Sangu amewataka wachezaji hao kuwa mfano katika mashindano hayo kwani yeyote atakayeonesha tabia mbaya atambue anaharibu taswira ya Ofisi yenye dhamana na Watumishi wa Umma nchini.
Naye Katibu Mkuu-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi ametumia fursa hiyo kuahidi kutoa donge nono kwa wachezaji mbalimbali watakaoibuka na ushindi katika michezo mbalimbali inayoendelea.
" Ongezeni juhudi ili mwaka huu mbali ya kuchukua ushindi wa mashindano ya baiskeli, tuchukue ushindi wa tufe, netiboli, kucheza karata pamoja mpira wa miguu" amesema Mhe.Sangu
" Naomba niwaahidi mkitwaa vikombe kwenye haya mashindano nitawapatia zawadi kwa hiyo pambaneni ili mrudi na ushindi" amesema Katibu Mkuu Mkomi.
Kufuatia hatua hiyo, Bw. Mkomi amewataka wachezaji hao kufanya mazoezi kwa kujituma ili waweze kurudi na ushindi huku akiwasisitiza kuwa anataka kuona thamani ya fedha inayotumika kuwahudumia iaki ushindi utakaopatikana
No comments:
Post a Comment