HAKIKISHENI WAHITIMU WA MAFUNZO YA POLISI JAMII WANAPEWA POSHO - SACP KATABAZI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, October 5, 2024

HAKIKISHENI WAHITIMU WA MAFUNZO YA POLISI JAMII WANAPEWA POSHO - SACP KATABAZI.


Na Carlos Claudio, Dodoma.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma SACP George Katabazi amehimiza serikali ya kata pamoja na polisi wa maeneo hayo kuandaa utaratibu maalum wa kuwalipa polisi jamii posho zitakazoleta motisha katika suala la utekelezaji wa ulinzi kwenye jamii.


SACP Katabazi ameyasema hayo jijini Dodoma katika hafla ya kufunga mafunzo ya polisi jamii shirikishi kata ya Chang’ombe na kutoa ahadi ya kufwatilia maadili pamoja na matendo ya wahitimu hao kupitia kazi za mafuzo waliyopata.


Amesema ataanzisha doria pamoja na polisi kata kukagua vikundi vyote shirikishi ndani ya mkoa wa Dodoma ili kuhakikisha kazi zinafanyika na vikundi hivyo vinakuwa endelevu kwa manufaa ya amani katika jamii.


“Nyinyi ni walezi, hivi vikundi vinaweza vikaanzishwa lakini je vinakuwa endelevu? vitafanya kazi? kama walivyokuwa wanatuonyesha ?Na hiyo ndiyo changamoto tunayoiona , niwaombe jamani mfanye kazi, mimi nitavikagua na wakati mwengine nitaingia doria na nyinyi,”


“Na niwaombe sasa, wale ambao mtaona hawafai wanaanza kukengeuka msikae nao kwenye hivi vikundi muwaondoe kabisa, muwe na sheria na kanuni za kuongoza hivi vikundi, mtu ambaye anakengeuka tumuondoe kwasababu muda mwengine yupo pale kwaajili ya kuchora dili na ramani tu.” amesema Katabazi.


Aidha ametoa maagizo kwa vikundi vya polisi jamii kutumia fursa ya mafunzo waliyopata ili kufichua na kutoa taarifa za waharifu katika mitaa wanayoishi.


Kwa upande wake diwani wa Chan’gombe Mhe. Bakari Samuel amesema kupitia mafunzo ya vijana hao kutabadilisha taswira ya kata ya Chan’gombe kwa uimarishwaji wa ulinzi pamoja na mali za wakazi wa kata hiyo.


Sambamba na hayo Mhe. Samuel amemuomba mkuu wa jeshi la polisi Dodoma kuwakumbuka vijana waliokuwa na vigezo katika suala la ajira kwani wahitimu wa awali wa kata ya Chan’gombe walikuwa na vigezo lakini hawakuweza kufanikiwa kupata ajira.


Nae mkaguzi msaidizi wa polisi kata ya Chan’gombe Samuel Gwivaha ameeleza ushirikiano alioupata kutoka kwa balozi wa kila shina na kufanikisha kuwapata vijana hao waliohitimu mafunzohayo kwa lengo la kupambana na uhalifa ndani ya kata ya Chan’gombe.


“Mpaka sasa kata ya Chan’gombe ni shuari, Chan’gombe watu wanalala milango wazi sasa hivi hakuna uhalifu kabisa kwasababu nina vijana zaidi ya sabini ambao nimewapa mafunzo haya ya uzalendo na nina shirikiana nao vizuri katika doria mbalimbali katika kata hii ya Chan’gombe, amesema Gwivaha.









.


No comments:

Post a Comment