SEPESHA RUSHWA YAJA NA MAKUBWA DODOMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, October 7, 2024

SEPESHA RUSHWA YAJA NA MAKUBWA DODOMA


Mkuu wa wilaya ya Dodoma Jabiri shekimweri amezindua kampeni ya kupinga Rushwa ijulikanayo kama Sepesha Rushwa, yenye lengo la kutoa elimu kwa makundi maalumu yanayoathirika na vitendo hivyo.

Mheshimiwa shekimweri amesema kampeni hiyo ina lengo la kumuunga mkuno Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambaye anamekuwa ni namba moja katika kupinga vitendo vya Rushwa ambavyo vimekuwa vikizorotesha maendeleo na upatikanaji haki.

Mheshimiwa Shekimweri amesema kampeni hiyo inalenga kutoa elimu mashuleni na kwa vijana mavyuoni ili wanapomaliza shule na vyuo wawe wanatambua maana ya Rushwa na inavyoweza kuwanyima haki yao katika nyanja mbalimbali

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi wa shirika la Sepesha Rushwa Dk Mbaga amesema hii ni mara ya tatu kufanyika kwa kampeni hiyo, ambayo huwa inafanyika kila mwaka toka kusajiliwa kwa shirika hilo, na mwaka huu itafanyika siku ya tarehe 1Desemba 2024 na wameanza mapema kwa kusajili watu kwa ajili ya kukimbia mbio za Marathoni itakayofanyika siku hiyo.

Ambayo itahusisha kukimbia mbio za kilomita kuanzia 5 , 10 na kIlimita 21 itakayofanyika siku ya Jumapili tarehe 1 December 2024.

Na pesa itakayopatikana kiasi kikubwa kitaelekezwa kwenye kampeni hiyo kwa ajili ya kutoa elimu.

No comments:

Post a Comment