TANESCO SHINYANGA YATOA ELIMU KUHUSU NISHATI SAFI YA KUPIKIA KWA KUTUMIA UMEME - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, October 9, 2024

TANESCO SHINYANGA YATOA ELIMU KUHUSU NISHATI SAFI YA KUPIKIA KWA KUTUMIA UMEME

Wananchi wakiendelea kupata elimu ya Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kwa kutumia umeme
Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Shinyanga, Victory Senge akitoa elimu kwa vitendo kuhusu Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kwa kutumia umeme

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Shinyanga limetoa elimu kwa vitendo kuhusu Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kwa kutumia umeme.

Akizungumza leo Jumatano Oktoba 9,2024 katika viwanja vya Ofisi za TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Shinyanga, Victory Senge amesema wametoa elimu hiyo sambamba na kutoa zawadi mbalimbali kwa wateja wa TANESCO ikiwa  ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.

“TANESCO Mkoa wa Shinyanga inaunga mkono 
jitihada anazofanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan  za kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia. Tumetoa elimu kuhusu Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kwa kutumia umeme namna ya kutumia umeme kidogo kwa kutumia majiko ya kisasa ya kupikia”,amesema Victory.

Victory amewahamasisha wananchi kutumia Nishati Safi ya Kupikia kwa kutumia nishati ya umeme kwa sababu inaokoa muda jikoni, ni salama kwa matumizi, hulinda afya, haitoi moshi, hutunza mazingira, inaimarisha usafi na hutumia kiasi kidogo cha umeme.

Nao baadhi ya wananchi wameishukuru TANESCO kwa kutoa elimu kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kutumia majiko sanifu ya umeme yenye presha ambayo ni majiko ya umeme yanayopika kwa kutumia joto na presha ya mvuke unaokusanywa ndani ya sufuria. 

Majiko sanifu ya umeme hutumia nishati kidogo sana na kuivisha chakula kwa muda mfupi na kuhifadhi virutubisho hivyo kuokoa fedha, muda, afya na mazingira lakini pia yana uwezo wa kupika vyakula mbalimbali kama vile makande, wali, ndizi, mchemsho, ugali,nyama, samaki, pilau n.k kwa njia ya kuchemsha, kurosti/kuunga, kwa mvuke (steam cooking), kukaanga (frying) na kuoka.

Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Shinyanga, Victory Senge akitoa elimu kwa vitendo kuhusu Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kwa kutumia umeme leo Jumatano Oktoba 9,2024 ikiwa ni Sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Shinyanga, Victory Senge akitoa elimu kwa vitendo kuhusu Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kwa kutumia umeme, kulia ni Afisa Uhusiano na Huduma kwa wateja TANESCO Shinyanga Robert Msemo
Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Shinyanga, Victory Senge akitoa elimu kwa vitendo kuhusu Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kwa kutumia umeme
Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Shinyanga, Victory Senge akitoa elimu kwa vitendo kuhusu Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kwa kutumia umeme

Wananchi wakiendelea kupata elimu ya Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kwa kutumia umeme
Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Shinyanga, Victory Senge akitoa elimu kwa vitendo kuhusu Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kwa kutumia umeme
Wananchi wakiendelea kupata elimu ya Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kwa kutumia umeme
Wananchi wakiendelea kupata elimu ya Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kwa kutumia umeme
Mteja wa TANESCO akiangalia bango la Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kwa kutumia umeme
Wananchi wakiendelea kupata elimu ya Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kwa kutumia umeme
Wananchi wakiendelea kupata elimu ya Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kwa kutumia umeme

Wananchi wakiendelea kupata elimu ya Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kwa kutumia umeme
Wananchi wakiendelea kupata elimu ya Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kwa kutumia umeme
Wananchi wakiendelea kupata elimu ya Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kwa kutumia umeme
Afisa Uhusiano na Huduma kwa wateja TANESCO Shinyanga Robert Msemo (kulia) akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wateja wa TANESCO

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

No comments:

Post a Comment