Meneja wa TANESCO Wilaya ya Kahama Mhandisi Kisika Eliya Kisika (kushoto) akimkabidhi cheti cha pongezi na Shukrani Meneja wa Kampuni ya Jema Africa Ltd, Sabina Machage
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Shinyanga imewatambua wateja wake wakubwa wilayani Kahama kwa kukata na kula nao keki pamoja na kuwapatia vyeti pongezi na shukrani kwa kulipa ankara za umeme kwa wakati.
Miongoni mwa wateja wakubwa waliopatiwa vyeti vya shukrani ni Domain Gold Plant, D4N Company Ltd, Jema Africa Ltd, Kayo Bigazaba (Mongo Elution Plant) na Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) ambako pia Wafanyakazi wa TANESCO wamekata na kula keki na wafanyakazi wa KACU.
Akizungumza leo Alhamisi Oktoba 10,2024 Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Shinyanga, Victory Senge akiwa ameambatana na maafisa wa TANESCO akiwemo Meneja wa TANESCO Wilaya ya Kahama Mhandisi Kisika Eliya Kisika amesema wametoa zawadi hizo ikiwa ni Sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja inayoongozwa na Kauli mbiu ‘Ni Zaidi ya Matarajio’.
“TANESCO Mkoa wa Shinyanga inawashukuru wateja wetu wakubwa wa umeme kwa namna mnavyoshirikiana nasi ikiwemo kulipa Ankara kwa wakati. Tunaendelea kuboresha huduma zetu mfano huduma ya Nikonekt inayowezesha kuomba huduma ya umeme hata ukiwa nyumbani na tumeongeza njia mpya ya huduma kwa wateja kupitia Whatsapp iitwayo Jisoti na TANESCO inayorahisisha mawasiliano ya huduma kwa mteja kupitia namba 0748550000”,amesema.
Nao wateja wakubwa wa TANESCO wameishukuru TANESCO kwa kuwatambua na kuwapatia vyeti huku wakiahidi kuendelea kushirikiana na shirika hilo la umeme.
Keki maalumu iliyoandaliwa na TANESCO Mkoa wa Shinyanga, kwa ajili ya Wateja Wakubwa Wilayani Kahama
Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Shinyanga, Victory Senge akizungumza na Wafanyakazi wa KACU wakati TANESCO ilipowatembelea Wateja Wakubwa Wilayani Kahama kisha kukata na kula nao keki pamoja na kuwapatia vyeti pongezi na shukrani kwa kulipa ankara za umeme kwa wakati.
Meneja wa TANESCO Wilaya ya Kahama Mhandisi Kisika Eliya Kisika akimlisha keki Meneja Uendeshaji wa KACU, Amiri Mwinyimkuu (kushoto)
Meneja Uendeshaji wa KACU, Amiri Mwinyimkuu akimlisha keki Meneja wa TANESCO Wilaya ya Kahama Mhandisi Kisika Eliya Kisika
Meneja wa TANESCO Wilaya ya Kahama Mhandisi Kisika Eliya Kisika akimkabidhi cheti cha pongezi na Shukrani Meneja Uendeshaji wa KACU, Amiri Mwinyimkuu
Meneja wa TANESCO Wilaya ya Kahama Mhandisi Kisika Eliya Kisika (kulia) akimlisha keki mmoja wa wafanyakazi wa KACU
Meneja wa TANESCO Wilaya ya Kahama Mhandisi Kisika Eliya Kisika (kulia) akimlisha keki mmoja wa wafanyakazi wa KACU
Meneja wa TANESCO Wilaya ya Kahama Mhandisi Kisika Eliya Kisika (kulia) akimlisha keki mmoja wa wafanyakazi wa KACU
Meneja wa TANESCO Wilaya ya Kahama Mhandisi Kisika Eliya Kisika, wafanyakazi wa TANESCO wakipiga picha ya kumbukumbu na wafanyakazi wa KACU
Meneja wa TANESCO Wilaya ya Kahama Mhandisi Kisika Eliya Kisika, wafanyakazi wa TANESCO wakipiga picha ya kumbukumbu na wafanyakazi wa KACU
Meneja wa TANESCO Wilaya ya Kahama Mhandisi Kisika Eliya Kisika (kushoto) akimkabidhi cheti cha pongezi na Shukrani Msimamizi wa ujenzi Yolanda Hotel inayomilikiwa na Domain Gold Plant, bw. Juma Kagame Nyerere
Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Shinyanga, Victory Senge akizungumza wakati wafanyakazi wa TANESCO walipotembelea Kampuni ya Domain Gold Plant
Wafanyakazi wa TANESCO wakipiga picha na mfanyakazi wa Kampuni ya Domain Gold Plant, Juma Kagame Nyerere.
Meneja wa TANESCO Wilaya ya Kahama Mhandisi Kisika Eliya Kisika (kulia) akimkabidhi cheti cha pongezi na Shukrani Mhasibu wa Kampuni ya D4N Company Ltd, Amasha Isack Kihomwe
Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Shinyanga, Victory Senge akizungumza wakati wafanyakazi wa TANESCO walipotembelea Kampuni ya D4N Company Ltd.
Meneja wa TANESCO Wilaya ya Kahama Mhandisi Kisika Eliya Kisika (kushoto) akimkabidhi cheti cha pongezi na Shukrani Meneja wa Kampuni ya Jema Africa Ltd, Sabina Machage
Meneja wa Kampuni ya Jema Africa Ltd, Sabina Machage akitoa neno la shukrani
Meneja wa TANESCO Wilaya ya Kahama Mhandisi Kisika Eliya Kisika (kushoto) akimkabidhi cheti cha pongezi na Shukrani Mhasibu wa Kampuni ya Kayo Bigazaba (Mongo Elution Plant), Sophia Mpina, kushoto ni Mhasibu wa TANESCO Wilaya ya Kahama, Mligo Gelard.
Meneja wa TANESCO Wilaya ya Kahama Mhandisi Kisika Eliya Kisika (kushoto) akimkabidhi cheti cha pongezi na Shukrani Mhasibu wa Kampuni ya Kayo Bigazaba (Mongo Elution Plant), Sophia Mpina.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
No comments:
Post a Comment