UNDP YANUFAISHA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, October 1, 2024

UNDP YANUFAISHA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI.

 



Na Jasmine Shamwepu,Dodoma.


SHIRIKA la maendeleo la umoja wa Mataifa UNDP limewajengea uwezo Taasisi na Mashirika yasiyo ya kiserikali kuziwezesha  kutekeleza miradi katika ngazi ya jamii ili kupambana na changamoto zinazoikumba Dunia.



UNDP inatekeleza program ya Mfuko wa mazingira Duniani (Small grants program)ambapo limekuwa likitoa ruzuku mbalimbali za utunzaji wa mazingira katika ngazi ya jamii.


Akizungumza na waandishi wa habari mratibu wa program ya mfuko wa mazingira duniani Faustine Ninga amesema UNDP inajengea uwezo taasisi za kijamii ikiwemo vikundi vya kijamii, Ngo’s uwezo wa kutekeleza miradi katika ngazi ya jamii pamoja na uwezo wa kupambana na changamoto ikiwemo uharibifu wa mali hasili, uhifadhi wa vyanzo vya maji, ukame, mabadiliko ya tabia nchi, kuboresha shughuli za kilimo na shughuli za ufugaji zinazosaidia katika kutunza  mazingira


Ninga amesema lengo la UNDP ni kuona taasisi hizo zisizo za kiserikali zinakuwa na uwezo wa kutekeleza miradi moja kwa moja kwa namna ambayo jamii inashiriki na itahamasika katika kufanya shughuli za uhifadhi wa mazingira pia kuwasaidia kuweza kuongeza kipato kupitia shughuli hizo za uhifadhi wa mazingira


“Ni program ambayo ilianza mwaka 1994 kwa hapa Tanzania na tumekuwa tukifanya kazi zaidi kwa kipindi cha miaka 15 iliyopita na tumejikita shughuli zetu katika nyanda kuu 3 upande wa Serengeti, upande wa Kilimanjaro na upande wa Jozani ambayo ipo upande wa Zanzibar.


“Kwa hivi karibuni mwaka huu mwanzoni tuliweza kuingia makubaliano na mashirika 44 ambayo yalipewa ruzuku ambayo inafikia karibia bilioni 4 kwaajili ya kutekeleza miradi ya jamii ili kuweza kuimarisha uwezo wa jamii wa kuweza kutunza mazingira lakini kujipatia kipato kupitia shughuli izo,” amesema Ninga.


Aidha amebainisha kuwa katika mashirika hayo wapo wazoefu na wasio wazoefu hivyo wanatambua uwezo wao na wanaendelea kuwajengea uwezo ili  mashirika yaweze kukuwa zaidi na kuweza kuelewa namna ya kuripoti mafanikio katika shughuli zao.


Kwa upande wake mkurugenzi wa TNRF Zakaria Faustine amesema wanashirikiana na UNDP ili kuijengea jamii uwezo mzuri wa kazi wanazozifanya pia uwezo wa kukamilisha majukumu kwa kina.


 Mkurugenzi wa TNRF, Zakaria Faustine amesema wanaridhishwa na kazi nzuri ambazo zinafanywa na taasisi zote zilizopewa ruzuku.


Amesema wamekutana na wanufaika wapya 43 wanaofadhiliwa na UNDP hivyo wanawapitisha katika miongozo mbalimbali ikiwemo uwezo wa kuandika ripoti, maeneo ya kuzingatia ambayo yatawapa matokeo bora ambayo yatapelekea utunzaji wa mazingira Tanzania.



Pamoja na hayo amesema wamepewa jukumu kuhakikisha kwamba wale wanufaika wote wanaopata pesa kupitia small grants wamejengewa uwezo wa kwenda kusimamia miradi 43 ya UNDP.


Sambamba na hayo amesema wanufaika hao kupitia program hiyo wataenda kunufaisha jamii kwenye sekta ya uchumi pamoja na utunzaji mzuri wa mazingira.


Nae mmoja wa washiriki wa warsha hiyo kutoka ummoja wa watu wenye ulemavu Zanzibar UWZ Mohamed Madaha amesema amenufaika kwa kujengewa uwezo wa namna ya kuandika ripoti ya matokeo ya miradi yao hivyo ameongeza uwezo wa kwenda kuongeza katika uandishi wake katika utekelezaji wa mradi wake.


Ameongeza kuwa mradi wake umegawanyika katika sehemu mbili ikiwa ufugaji wa nyuki na nzi maalumu wa kilimo cha `Black Soja Fly’ wanaotambulika kama nzi chuma ambayo kazi zao ni kusafisha mazingira, kutoa ajira kwa vijana kwenye miradi pamoja na uzalishaji wa mbolea kwa manufaa ya wakulima kupunguza matumizi ya kemikali kwenye kilimo.


Mfuko wa Mazingira Duniani(GEF) kupitia Programu ya Ruzuku Ndogo inayotekelezwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)  umetoa zaidi ya sh  4.04  bilioni kwa mashirika yasiyo ya kiserikali zaidi ya 44 nchini ili kutekeleza miradi ya Uhifadhi wa Mazingira, Misitu, kuendeleza ufugaji nyuki, kutunza vyanzo vya Maji na uwezeshaji Jamii kiuchumi.








No comments:

Post a Comment