WAJASIRIAMALI WADOGO WATAKIWA KURASIMISHA BIASHARA ZAO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, October 24, 2024

WAJASIRIAMALI WADOGO WATAKIWA KURASIMISHA BIASHARA ZAO



Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe (Mb) akiangalia bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali walionufaika na mafunzo yanayoendwa na SIDO kwenye viwanja vya maonesho ya 'Tanzanite Manyara Trade Fair 2024' (Stendi ya zamani ya mabasi-Babati) Oktoba 23, 2024 mkoani Manyara.

......

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe ametoa wito kwa Wajasiliamali wadogo kurasmisha biashara zao na kulipa kodi kwa hiari ili kukuza biashara zao, kuchangia katika Pato la Taifa na kuiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kati wa juu.

Vilevile, ametoa wito kwa Mamlaka za udhibiti na usimamizi wa biashara nchini kuboresha utendaji kazi, kuisaidia sekta binafsi ili ikue na kuwa sekta kiongozi katika kutoa ajira na kuongeza pato la Taifa na si kuikwamisha kwa kuwafungia biashara hususani Wajasiriamali wadogo ambao hawajatimiza vigezo vya kisheria au kukosea katika kuanzisha na kuendeleza biashara zao.

Kigahe ametoa wito huo Oktoba 23, 2024 alipokuwa akizindua Maonesho ya Biashara, Madini, Viwanda na Kilimo ya Tanzanite Manyara Trade Fair 2024 yanayofanyika mjini Babati mkoani Manyara kuanzia tarehe 20 hadi 30 Oktoba 2024 yakiongozwa na kauli mbiu isemayo "Manyara kwa Ustawi wa Biashara na Uwekezaji."

Aidha amebainisha kuwa Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya biashara, kuhuisha Sera, Sheria na Mikakati mbalimbali inayoleta vikwazo katika ufanyaji biashara ili kukuza biashara, kuvutia wawekezaji na kujenga uchumi wa nchi kwa ujumla.

Kigahe pia ameisistiza kuimarisha ushirikiano baina ya Serikali na Sekta binafsi pamoja na kubadilisha fikra na vitendo potofu katika biashara pamoja na kuzingatia utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi pale wanapoanzisha viwanda .

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Emmanuella Kaganda Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara ametoa wito kwa wajasiliamali na wawekezaji katika mkoa huo kutumia na kutangaza fursa mbalimbali zilizopo hususani katika sekta za utalii, kilimo, madini na maeneo mengine muhimu.

Naye Katibu Mtendaji wa Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Mkoa wa Manyara Bi Zainabu Rajabu amebainisha kuwa maonesho ya mwaka 2024 yamehudhuriwa na washiriki 337 ndani na nje ya nchi na washiriki hao wamepata fursa ya kubadilishana uzoefu, kujifunza na kupata wateja.


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe (Mb) akikabidhiwa zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Utafiti wa mbogamboga (World Vegetable Center), Bi. Colleta Ndunguru kwenye viwanja vya maonesho ya 'Tanzanite Manyara Trade Fair 2024' (Stendi ya zamani ya mabasi-Babati) Oktoba 23, 2024 mkoani Manyara.


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe (Mb) akiangalia bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali walionufaika na mafunzo yanayoendwa na SIDO kwenye viwanja vya maonesho ya 'Tanzanite Manyara Trade Fair 2024' (Stendi ya zamani ya mabasi-Babati) Oktoba 23, 2024 mkoani Manyara.


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe (Mb) akisikiliza maelezo kutoka kwa mjasiriamali wa kutoka nchini Uganda , Bi. Namara Sarah alipowasili kwenye banda hilo la bidhaa za Uganda kwenye viwanja vya maonesho ya 'Tanzanite Manyara Trade Fair 2024' (Stendi ya zamani ya mabasi-Babati) Oktoba 23, 2024 mkoani Manyara.

No comments:

Post a Comment