WAZIRI STERGOMENA TAX AKABIDHIWA JEZI YA TIMU YA MASHUJAA FC - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, October 2, 2024

WAZIRI STERGOMENA TAX AKABIDHIWA JEZI YA TIMU YA MASHUJAA FC


Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb), tarehe 02 Oktoba 2024, amekabidhiwa Jezi ya Timu ya Mpira wa Miguu ya Jeshi la Ulinzi wa Wananchi Tanzania, maarufu kama Mashujaa.

Hafla hiyo fupi ya kumkabidhi Jez Waziri wa Ulinzi na JKT, imefanyika Ofisi ndogo za Wizara ya Ulinzi na JKT, Upanga Jijini Dar Es salaam, ambapo Waziri Tax imekabidhiwa jezi hiyo na Mwenyekiti wa Mashujaa FC, Kanali Benjamin Kisinda, ikiwa ni kutambua mchango wa Dkt Stergomena Tax katika kukuza na kuendeleza sekta ya Michezo katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na timu za Wizara ya Ulinzi kwa ujumla.

Akizungumza katika hafla hiyo fupi ya Kukabidhiwa jezi, Dkt. Tax amewataka Timu ya Mashujaa pamoja na Timu zote zilizo chini ya Wizara na JWTZ kuhakikisha zinaendelea kushindana na kushinda ili kufikia malengo ya Wizara na Taifa kwa ujumla na akawakumbusha kuwa Michezo ni Afya,Burudani na ajira pamoja na kuimarisha afya ya akili.

Waziri wa Ulinzi na JKT amewahakikishia wachezaji na viongozi wa Timu ya Mashujaa kuwa Wizara ipo nyuma na timu zote za Wizara kuhakikisha timu hizo zinafikia malengo yake kitaifa na kuiwakilisha nchi Kimataifa

No comments:

Post a Comment