Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Dar es Salaam inatekeleza mradi wa matengenezo (maintenance) ya miundombinu ya mabasi yaendayo haraka (BRT) awamu ya kwanza chini ya mradi wa OPBRC (Output and Performance-Based Road Contract) uliosainiwa rasmi tarehe 07 Septemba 2018.
Mradi huu ni wa muda mrefu (Long term contract) ulianza rasmi tarehe 01 Aprili 2019 ukitekelezwa na mkandarasi M/s Bharya Engineering & Contracting Co. Ltd (BECCO) kwa utekelezaji wa mradi kwa muda wa miezi sitini (60) yaani miaka mitano (5).
Hayo yamebainishwa na Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi John Mkumbo leo tarehe 5 Novemba 2024 na kueleza kuwa mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 18.509 ambazo zinajumuisha makundi matatu ya kazi.
Ameyataja makundi hayo kuwa ni Pamoja na Mradi wa matengenezo ya miundombinu ya mabasi yaendayo haraka (BRT) awamu ya kwanza yenye urefu wa kilomita 21.4 ikihusisha: Barabara ya Morogoro kuanzia Ferry mpaka Kimara Mwisho, Barabara ya Kawawa (Magomeni Mapipa – Morocco); na Barabara ya Msimbazi (Fire – Msimbazi BRT Station).
Mhandisi Mkumbo amesema kuwa TANROADS pia inatekeleza kazi za maboresho ya sehemu zilizoharibika (Rehabilitation works) ikihusisha Matengenezo makubwa ya tabaka la lami katika sehemu zilizokuwa zimeharibika. Maeneo yaliyofanyiwa marekebisho ni Ubungo maji, Kibo, Corner, Baruti, Bucha, Korogwe na Kimara Mwisho. Tabaka la lami katika maeneo haya liliondolewa (milling) pamoja na kuwekwa lami mpya kwa kutumia technolojia ya Superpave (SP 12.5), Kuweka nguzo za zege (precast concrete poles C20/guard posts), Ujenzi wa sehemu za watembea kwa miguu (paving blocks), Ujenzi wa kingo za barabara (Kerbstones) na Matengenezo kwenye njia za waendesha baiskeli.
Pia TANROADS Dar es salaam imefanya kazi za dharula (Emergency works). Kazi hizi zinahusisha matengenezo ya uharibifu ambao haukutarajiwa (unforeseable events that are beyond the control). Kazi hizi ni pamoja na; Kuondoa tope, mchanga na takataka kwenye daraja na eneo la barabara wakati wa mafuriko na mvua kubwa, na Matengenezo ya miundombinu yatokanayo na ajali za barabarani kwenye miundombinu ya BRT awamu ya kwanza.
Mhandisi Mkumbo ameeleza kuwa kazi za matengenezo zimefanyika wakati wote (OPBRC maintenance works). Kazi hizi zinahusisha; Urudishiaji wa michoro ya barabara (road marking), Uwekaji wa alama za barabarani (road signs), Matengenezo/uzibuaji wa mitaro ya maji ya mvua (underground drainage systems) ndani ya uwanda wa km 21.4 za mradi, Kuweka mifuniko ya zege kwenye mifumo ya maji (chambers), Kuondoa mchanga kwa kufagia barabara ndani ya Km 21.4 kila siku.
Kazi zingine ni Pamoja na Kufyeka majani na kutunza maeneo yenye bustani (green areas) ndani ya eneo la mradi, Kuondoa vichaka na kupunguza miti (prunning) iliyo pembezoni mwa barabara (road reserve), Kuziba viraka/mashimo, Matengenezo madogo ya madaraja yaliyopo ndani ya mradi, Marekebisho ya njia za waenda kwa miguu/baiskeli, Matengenezo ya nguzo za zege zinazoharibika, Matengenezo ya maungio ya zege (joint sealing), Marekebisho ya mifuniko (catchpit grating), na Kuzibua mifereji yote iliyo kwenye eneo la mradi.
No comments:
Post a Comment