Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Novemba 18, 2024 jijini Dar es Salaam amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian, kuhusu namna ya kuimarisha ushirikiano katika masuala ya elimu, hususan elimu ya amali ufundi.
Waziri Mkenda ameeleza kuwa Serikali kupitia Wizara inaendelea kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mageuzi ya elimu, ikiwa ni pamoja na kuweka nguvu kuimarisha elimu ya amali ufundi inayolenga kuwezesha ujuzi kwa vijana.
Amesema China na Tanzania zina historia chanya ya ushirikiano katika sekta ya elimu, na kwamba Serikali ina shauku kubwa kushirikiana na nchi hiyo katika kuwezesha utekelezaji wa mafunzo ya ufundi nyanja za uhandisi.
Mhe. Chen amesema Serikali ya China inajivunia ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa fursa za mafunzo katika Elimu ya ufundi ambao unalenga kukuza viwango vya ujuzi na umahiri kwa vijana.
Ameipongeza Serikali chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusimamia kikamilifu mageuzi ya elimu.
No comments:
Post a Comment