Na. MWANDISHI WETU
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania TACAIDS kujadili kuhusu maandalizi ya Maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani ambayo inaadhimishwa kila mwaka ifikapo Disemba Mosi.
Dkt.Yonazi amekutana na uongozi huo Ofisini kwake Jijini Dodoma tarehe 01 Novemba, 2024 ambapo
kikao hicho kilihudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Anderson Mutatembwa pamoja na timu ya wataalam kutoka Idara ya Sera na Uratibu wa Shughuli za Serikali katika Ofisi hiyo.
No comments:
Post a Comment