JITIHADA ZA DUWASA ENEO LA KISASA YAANZA KUZAA MATUNDA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, November 21, 2024

JITIHADA ZA DUWASA ENEO LA KISASA YAANZA KUZAA MATUNDA



Na Okuly Julius _Dodoma


Juhudi za Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) ya kuhakikisha wananchi wa eneo la Kisasa wanapata maji safi na salama sasa zimefanikiwa.

Ambapo zoezi la kusafisha maji kwa lengo la kusambazwa kwa wananchi limefanyika leo Novemba 21,2024 likiongozwa na Mkurugenzi wa usambazaji maji na Usafi wa Mazingira DUWASA, Mhandisi Bernard Rugayi

Mhandisi Bernard Rugayi amesema Mradi wa Uboreshaji Huduma ya Maji Kisasa-Mwangaza umefikia asilimia 95 ya utekelezaji na kwamba baadhi ya wananchi wa maeneo ya Kisasa, Mwangaza na Nyumba 300 jijini Dodoma wataanza kupata Huduma ya Maji leo Novemba 21, 2024.

Mhandisi Rugayi amewahakikishia wananchi wa maeneo hayo leo Novemba 21,2024 kuwa watapata huduma ya maji kwa saa 24.

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) inatekeleza mradi wa kuboresha huduma ya maji eneo la Kisasa ambako kumechimbwa kisima kirefu cha mita 152 chenye uwezo wa kuzalisha maji lita milioni 2.88 kwa siku.






No comments:

Post a Comment