Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira inayoongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Jackson Kiswaga (Mb) imekagua miradi ya maji Hanang na kuridhishwa na utekelezaji wake.
Mhe Kiswaga amesema miradi yote iliyokaguliwa na hasa mradi wa kurudisha huduma kwa wananchi wa Hanang kupitia wataalam wa ndani umefanyika kwa ubora na hivi sasa wananchi wanapata huduma ya maji kwa asilimia 92.
Kamati hiyo imekagua ujenzi wa chanzo cha Maji cha Mlima Hanang', ujenzi wa Mitambo ya kuchuja na kutibu maji ( Jorodom), ujenzi wa chanzo na kuunganisha maji katika Nyumba 108( Wareti) na mradi wa maji na Point Source Sarjanda na Kinyamburi.
Mhe. Kiswaga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kufanikisha miradi hiyo kwa kutoa fedha.
No comments:
Post a Comment