MATUKIO KATIKA PICHA : Ziara ya IFAD na AFDP Katika Utekelezaji wa Programu ya Kilimo Wilayani Kilosa - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, November 7, 2024

MATUKIO KATIKA PICHA : Ziara ya IFAD na AFDP Katika Utekelezaji wa Programu ya Kilimo Wilayani Kilosa


Ujumbe kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) na wataalam kutoka Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu wametembelea Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) katika kituo cha Ilonga Wilayani Kilosa Mkoa wa Morogoro, ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya kutembelea maeneo yanayotekeleza Programu hiyo,Tarehe 7 Novemba 2024.

Ujumbe Huo Ulitembelea Bwawa litakalotumika katika kilimo cha Umwagiliaji wa Shamba la Wakala wa Mbegu za Kilimo Nchini (ASA) Msimba Wilayani humo Pamoja na kujionea mtambo mkubwa wa kuchakata mbegu.

Awali, Ujumbe huo Ulizungumza na Mkulima mdogo wa Uzalishaji wa mbegu katika kata ya Ulaya Wilayani Humo.




No comments:

Post a Comment