MBUNGE NJEZA AIBANA SERIKALI KUHUSU FIDIA KWA WANANCHI WANAOPISHA UJENZI WA BARABARA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, November 8, 2024

MBUNGE NJEZA AIBANA SERIKALI KUHUSU FIDIA KWA WANANCHI WANAOPISHA UJENZI WA BARABARA.

 


Na Saida Issa,Dodoma.

SERIKALI imesema kuwa iko katika utaratibu wa kulipa fidia kwa wananchi ambao wanapisha barabara ya mchepuko ya uyole_songwe 


Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Ujenzi Godfrey Kasekenya alipokuwa akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na Mbunge wa Mbeya Vijijini Oran Njeza alipouliza 

Je,ni lini Serikali italipa fidia kwa wananchi wanaopisha barabara ya mchepuo ya uyole-songwe bypass. 


"Kama tayari tumeshafanya tathmini wale ambao wako kwenye alama za kijani watalipwa na wale ambao wamewekewa alama nyekundu mana yake hawaatahili kulipwa, 


Nanimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tukishafanya tathimini sisi kama wizara tunawasilisha hayo madai ama hizo fidia wizara ya fedha ambao barabara zote zilizowekewa alama mana yake taarifa ziko wizara ya fedha na wanaendelea kutafuta fedha ili kabla ya ujenzi kuanza wananchi hao watalipwa fedha zao,"alisema.







No comments:

Post a Comment