Jukumu la kuhakikisha mtoto anakuwa salama mtandaoni ni la jamii nzima, hivyo iwapo mtoto akifanyiwa vitendo vya ukatili au kuhisi dalili za kufanyiwa ukatili wasisite kutoa taarifa ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.
Akitoa elimu hiyo kwa umma, Bw. Amos Mpili, Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum amesema matukio hayo ya ukatili dhidi ya watoto mtandaoni yanaweza kupunguzwa au kukomeshwa iwapo yataripotiwa na hatua stahiki kuchukuliwa.
Mosi, Mtoto anatakiwa kutoa taarifa kwa mzazi au mlezi au ndugu yeyote anayemuamini iwapo atakuwa amefanyiwa vitendo vya ukatili au kuna dalili za kufanyiwa vitendo hivyo.
Pili, Kuripoti katika madawati ya ulinzi na usalama wa mtoto shuleni
Tatu, Kuripoti katika vituo vya polisi kupitia dawati la jinsia na watoto
Nne, kupiga Namba Ya Bure 116 bila malipo kwa mitandao yote Tanzania kwa ajili ya kuripoti matukio ya ukatili dhidi ya watoto.
No comments:
Post a Comment