Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) Prof. Najat Kassim Mohammed amesema michezo ni muhimu kwa wafanyakazi katika kuongeza ufanisi kazini na kukuza maendeleo ya taifa kwa kuwa na nguvu kazi imara.
PROF. Najat ameyasema hayo katika ofisi za TAEC makao makuu jijini Dodoma wakati akiwapongeza wafanyakazi wa TAEC waliofanya vizuri katika mashindano ya michezo ya Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) michuano iliyofanyika jijini Tanga.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya michezo ya TAEC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Teknolojia ya Nyuklia na Huduma za Ufundi Dkt. Remigius Kawala amesema TAEC itaimarisha michezo mahali pa kazi kwa kila kanda.
Katika mashindano ya SHIMMUTA 2024 TAEC ilifanikiwa kupata jumla ya medali nne (4) ikiwemo tatu (3) za dhahabu na moja ya fedha (1) ikiwa ni ongezeko la medali 3 za dhahabu ambayo ni sawa na asilimia 100% ya medali za dhahabu ukilinganisha na matokeo ya SHIMMUTA 2023 yaliofanyika mkoani Dodoma.
Taasisi 95 zilishiriki mashindano ya SHIMMUTA 2024 ambapo jumla ya washiriki 4720 kutoka Taasisi za Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni binafsi walishiriki katika michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa pete, kuvutana kamba, riadha kukimbia na magunia na michezo ya jadi.
No comments:
Post a Comment