Na Okuly Julius _ DODOMA
Wananchi wametakiwa KUPAZA SAUTI kukemea na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi juu ya madereva wanaovunja sheria za usalama Barabarani ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa dereva husika lengo likiwa ni kuzue ajali barabarani.
Akizungumza wakati wa Katika Kampeni maalum ya "ABIRIA PAZA SAUTI" iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani (RSA), iliyokwenda sambamba na utoaji wa elimu kwa abiria na madereva katika kituo Kikuu cha Mabasi Nanenane Jijini Dodoma, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Boniphace Mbao amesema suala la usalama barabarani ni jukumu la kila Mtu.
"madereva tumeshawafundisha Sana sasa kazi inabaki kwenu abiria kusaidia kutoa taarifa juu ya madereva wanaokiuka sheria za usalama Barabarani kwani wananchi mna jukumu kubwa la kuhakikisha usalama barabarani unakuwepo,"
Na kuongeza kuwa " unapoulizwa na Askari hali ya safari ipoje jibu kama kuna tatizo Sema ili lishughulikiwe mapema kwani ukiacha kutoa taarifa ajali ikitokea na wewe unadhurika hivyo jukumu la usalama barabarani ni letu sote, "amesisitiza ACP Mbao
Pia amewataka madereva kuepukana na tabia ya kutumia Vilevi wakati wakiwa barabarani kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na inaweza kuwa chanzo cha ajali ambacho kinaweza kuzuilika
Kwa upande wake Mratibu wa Mabalozi wa Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma (RSA) Faustine Martina amewetaka abiria kuepukana na tabia ya kusimama kwenye basi kutokana na kukosa nafasi ya kukaa.
" ukuona dereva anaendesha mwendo ambao hamuuelewe muiteni hata kondakta muambieni kwa sababu ikitokea ajali wewe ndio utakayeathirika na hii tabia ya kusimama kwenye mabasi kwa sababu limejaa sio nzuri maana ikitokea ajali bima haitakutambua wewe uliyesimama, "ameeleza Martina
Naye , Balozi wa Usalama barabarani Mkoa wa Dodoma Joseph Nuru ameeleza lengo la Kampeni hiyo kuwa ni kuwakumbusha abiria nafasi yao katika kukabiliana na ajali za barabarani.
" KAMPENI YA "ABIRIA PAZA SAUTI" ni mahususi kabisa kwa ajili ya kuwakumbusha abiria kuwa wana wajibu wa kushiriki katika mapambano dhidi ya ajali za barabarani kwani dereva anavyofanya makosa abiria wakachukua jukumu la kutoa taarifa kwa Polisi na hatua zikachukuliwa basi itasaidia hata wengine kutotenda makosa, "amesema Nuru
No comments:
Post a Comment