Mke wa mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda anayezuiliwa Kizza Besigye ameshutumu kuwa ni "ukatili na unyama" wa kupiga marufuku wafungwa kupokea wageni siku ya Krismasi.
Besigye, 68, ameshtakiwa katika mahakama ya kijeshi kwa kupatikana na bastola na kujaribu kununua silaha nje ya nchi, jambo ambalo amekanusha. Kesi yake imeahirishwa hadi mwezi ujao.
Mamlaka ya magereza inasema kama sehemu ya hatua za kuzuia "kutokuwepo kwa usalama", wafungwa hawataruhusiwa kutembelewa na wageni kwa siku saba, kuanzia mkesha wa Krismasi.
Mkewe Besigye, Winnie Byanyima, mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na VVU na Ukimwi, alisema anapanga kupiga kambi nje ya Gereza la Luzira ili aweze kumuona mumewe na kumpa chakula siku ya Krismasi.
Mkewe Besigye, Winnie Byanyima, mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na VVU na Ukimwi, alisema anapanga kupiga kambi nje ya Gereza la Luzira ili aweze kumuona mumewe na kumpa chakula siku ya Krismasi.
Aliiambia BBC kwamba mume wake bado ni "mwenye nguvu na mvumilivu" katika "chumba kidogo " nyuma ya milango sita ya gereza, lakini alikuwa na wasiwasi kwamba anaweza "kudhurika".
"Siachi chakula cha Besigye langoni [kama nilivyoelekezwa]. Nitaenda huko na kumuona mume wangu kwa sababu siwaamini hata siku moja," Bi Byanyima alisema.
"Labda nitachukua hema na kulala huko ... ikiwa ndivyo wanataka," aliongeza.
Besigye amegombea na kushindwa katika chaguzi nne za urais dhidi ya Rais Yoweri Museveni, ambaye amekuwa madarakani tangu 1986.
Lakini mwanasiasa huyo mkongwe wa upinzani amekuwa hajishughulishi sana na siasa katika miaka ya hivi karibuni, na hakugombea uchaguzi wa 2021.
Besigye, hata hivyo, alirejea kwenye vichwa vya habari mwezi uliopita baada ya kutekwa nyara vibaya akiwa ziarani Kenya na kupelekwa Uganda kwa nguvu.
Kisha alishtakiwa pamoja na msaidizi, wake Obeid Lutale. Yeye, pia, amekanusha mashtaka.
CHANZO BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment