COOP BANK KUSHIRIKI KUTEKELEZA AJENDA YA KILIMO 10/30 KWA KUFADHILI MIRADI YA KIMKAKATI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, January 29, 2025

COOP BANK KUSHIRIKI KUTEKELEZA AJENDA YA KILIMO 10/30 KWA KUFADHILI MIRADI YA KIMKAKATI




Na Okuly Julius _Dodoma


BENKI ya Ushirika Nchini (COOP BANK) ,kwa kushirikiana na Serikali inatarajia kutekeleza Ajenda ya Kilimo ya 10/30 kwa kutoa huduma za kibenki na kufadhili miradi ya kimkakati ya Serikali ,vyama vya ushirika, makampuni ya mbolea (TFC), Bodi ya Tumbaku (TTB), zana za kilimo na Benki ya Serikaili ya Kilimo (TADB) ili kuongeza tija ya kilimo kitaifa kufikia asilimia 10 na kuwafikia wadau na wakulima wengi zaidi nchini ifikapo mwaka 2030.

Hayo yameelezwa leo Jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyi,Godfrey Ng'urah wakati akizungumza na Waandishi wa Habari pamoja na Wadau mbalimbali kuhusiana na shughuli zinazofanywa na Benki hiyo.

Aidha,Mkurugenzi huyo,amebainisha kuwa kwa kuwekeza katika misingi na miundo mbinu ya TEHAMA , Benki ya Ushirika itakuwa sio tu Benki, bali itakuwa Benki ya Tehama, inayotoa huduma za kibenki kwa umma wa watanzania na kwa gharama nafuu ili kukuza ujumuishi wa kifedha katika sekta zingine zilizonyuma kiuchumi.

"Kwa kuwekeza kwenye TEHAMA Ikichagizwa na uwepo na msukumo mkubwa wa kiserikali kujenga uchumi wa kidijitali- (Digital Economy) tutafanya uwekezaji mkubwa katika mifumo ya kutoa huduma za kibenki kidijitali ikiwa ni pamoja na mfumo mama wa kibenki (CBS) Mifumo ya akili bandia ( AI & Robotics technologies) mifumo ya utambuzi na kupata taarifa za wateja na mazoea yao (Machine Learning), mifumo ya kutunza kanzi data hewani (Cloud computing), Huduma za kibenki zilizojengwa juu ya shuguli za kidigitali ( Digital Banking) na uchumi ya takwimu (Big data analytics na Data monitizations) , huduma za benki kwa simu, (mobile banking) na huduma za uwakala ya kibenki, (Agency banking), "ameeleza Ng'urah

Pia amesema Benki hiyo imekuza kitabu chake cha mikopo toka shillingi milioni 320 mwaka 2020, hadi kufikia shillingi bilioni 15 mwaka 2024, sawa na ukuaji wa zaidi ya asilimia 5,000.

Hata hivyo, Benki imeimarisha ubora wa mikopo yake, huku mikopo chechefu ikipungua toka asilimia (74%) ya mwaka 2020 hadi kufikia asilimia 2% kwa mwaka 2024
Vilevile, amana za wateja zimeongezeka na kufikia bilioni 18 mwaka 2024 toka Bilioni 6 mwaka 2020, sawa na ukuaji wa asilimia 216% ndani ya miaka 4 ya mageuzi.

Aidha jumla ya rasilimali za Benki zimekuwa na kufikia shilingi bilioni 50, mwaka 2024, toka shilingi bilioni 9.5, mwaka 2020, sawa na ukuaji wa asilimia 733%. Hii ni spidi ya Tai, au mwanga kama utapenda kuita hivyo. Na kwa hakika bado, tutawaonyesha watanzania, huduma za Benki zinawezekana kwa kila raia wa wa nchi hii na sio kwa watu wachache tu.

Akizungumza katika Mkutano huo,Mrajis wa Vyama vya Ushirika Nchini,Dk.Benson Ndiege amesema kuwa ujio wa Benki hiyo unaenda kuchagiza maendeleo ya Ushirika katika kukuza uchumi.

"Sasa nitoe wito kwa wana ushirika kwamba sasa Benki ipo na tuendelee kuitumia kwa huduma za Ki Benki".

"Lakini wana ushirika nichukue nafasi hii kuwapongeza wanaushirika nchi nzima kwa kazi kubwa ambayo mmeifanya kwasababu maono haya mwanzoni mwa mwaka 2019 watu hawakuamini kwamba hili litatokea lakini wanaushirika walisimama kidete na Leo tumefika hapa, nawapongeza sana Wanaushirika na tuendelee kuchapa kazi".

Uanzishwaji wa Benki hii ni miongoni mwa matokeo ya kimkakati ya Wizara ya Kikimo chini ya uongozi imara wa Mhe Waziri Mohamed Hussein Bashe aliyedhamilia kufanya mapinduzi ya kilimo kupitia sekta ya usharika kujiendesha kibiashara kupitia Benki mwamvuli wa wa kisekta itakayojibu changamoto za upatikanaji mitaji ya kilimo kwa wakulima.

No comments:

Post a Comment