TUENDELEE KUSIMAMIA UTEKELEZAJI KAZI WA WALIMU KATIKA MAENEO YETU -DKT. SHINDIKA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, January 30, 2025

TUENDELEE KUSIMAMIA UTEKELEZAJI KAZI WA WALIMU KATIKA MAENEO YETU -DKT. SHINDIKA



OR - TAMISEMI

Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Elimu, Ofisi ya Rais - TAMISEMI Dkt. Emmanuel Shindika amewataka Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya kuendelea kusimamia utendaji kazi wa walimu ili kufanikisha jitihada za Serikali katika kutoa elimu.

Dkt. Shindika ameyasema hayo tarehe 29 Januari, 2025 Mkoani Singida wakati akifunga kikao Kazi cha Kutathmini Utekelezaji wa Shughuli za Elimu kuanzia mwezi Julai hadi Desemba 2024 kwa Wasaidizi wa Mikoa (ELIMU), Wakuu wa Divisheni za Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari.

“pamoja na upungufu wa walimu uliopo hasa katika Halmashauri za vijijini tuendelee kusimamia utendaji kazi wa walimu waliopo na kuimarisha mahusiano mazuri kazini ikiwa pamoja na kuwalipa stahiki zao na malipo ya likizo” alisema Dkt. Shindika.

Amesema dhamana waliyopewa ni kubwa ya kufanya na kusimamia majukumu hayo ili kupunguza changamoto Kwa walimu hao.

Aidha, amewataka viongozi hao kufanya tathmini mbalimbali mara baada ya matokeo ya mitihani kutangazwa na kuhakikisha mitihani ya upimaji kitaifa wanafanya vema kwa kubaini changamoto mbalimbali katika maeneo yao.

Naye Mwenyekiti wa Maafisa Elimu Mwl. Juma Kaponda ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuimarisha na kuboresha Sekta ya Elimu, ameongezea kwa kusema wataendelea kufanya kazi na kutekeleza yote yaliyo azimiwa katika kikao hicho.



No comments:

Post a Comment