
Na Okuly Julius _DODOMA
Serikali imelipa bilioni 254 ndani ya miezi miwili kwa wakandarasi wote wanaotekeleza Miranda ya ujenzi wa barabara ili warudi kwa ajili ya kukamilisha miradi hiyo.
Ambapo amesema kuwa Mkandarasi anayejenga barabara ya Ntyuka anadai bilioni zaidi ya sita kwa ajili ya mradi huo, atalipwa fedha hizo zote ndani ya mwezi huu wa pili ili arudi na kukamilisha mradi huo.
Kuhusu fedha za fidia kwa wananchi ambazo ni bilioni 7.4 Waziri Ulega amesema hatua zote za kisheria zikamilishwe ili wananchi hao waweze kulipwa.
"Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa pesa nyingi na fedha hizo zinatumika katika utekelezaji wa miradi na huu ni moja ya mradi na ndio maana ndani ya miezi miwili ametoa bilioni 254 kwa ajili ya kukamilisha miradi yote," amesema Ulega

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amesema Dodoma ina mtandao wa barabara za lami 249.9 KM
Katika kata 41 zilizopo ndani ya Wilaya ya Dodoma Mjini ila bado kuna changamoto ya kutoka kata moja kwenda nyingine.
"Tunaomba barabara hii ya Ntyuka ikamilike kwa kiwango cha lami ili kuwapunguzia adha wakazi wa Ntyuka ya kusafiri kutoka hapa kwenda mjini nauli inakuwa kubwa wakati mjini sio mbali, pia hospitali ya DCMC ambayo imekuwa ikipokea wagonjwa wengi hata kutoka nje ya Mkoa wa Dodoma, "amesema Mavunde
Pia ameomba wananchi wanaoguswa na barabara hiyo walipwe fidia kwani ni moja ya Changamoto inayowakabili.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri amesema Wananchi zaidi ya 200 wamepata ajira wakati ujenzi wa barabara hiyo ilivyoanza kujengwa na Mkandarasi atakaporudi kuendelea na ujenzi huo sio tu faida ya kukamilika kwa barabara bali hata wakazi Ntyuka watapata fedha na kujenga uchumi wao.





No comments:
Post a Comment