ERB YAWEKA LENGO KUFIKIA 50 KWA 50 KATIKA FANI YA UHANDISI IFIKAPO 2030 . - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, February 22, 2025

ERB YAWEKA LENGO KUFIKIA 50 KWA 50 KATIKA FANI YA UHANDISI IFIKAPO 2030 .


Msajili wa Bodi ya Wahandisi nchini (ERB), Mhandisi Bernard Kavishe amesema bodi hiyo ina sera maalum ya kutoa upendeleo chanya ili kumuongezea fursa mwanamke hususani wa fani ya uhandisi.

Kavishe ameyasema hayo wakati wa mahafali ya wanawake 15 waliosomeshwa na Bodi hiyo kupitia ATE kwa lengo la kuwawezesha wanawake hao wahandisi kuwa na sifa ya kuwa viongozi katika taasisi zao.

"ERB tunaamini katika usawa wa kijinsia, na katika kufikia shabaha hii, jinsia zote hazina budi kushirikiana, ndio ikazaliwa dhana ya kinababa, He for She, kwani tuna uhaba mkubwa wa wanawake wahandisi hapa nchini, kwani kwa kila mwanamke mmoja mhandisi, wapo wanaume saba wahandisi".Amesema Kavishe.

Mhandisi Kavishe amesema kuwa kati ya wahandisi karibu 42,000 waliosajiliwa na ERB wanawake wahandisi wapo takribani 6,000 pekee, kiwango kisichokubalika, ambacho kinahitaji kuwekewa mikakat ili kuongeza idadi ya wanawake katika fani ya uhandisi kifikia usawa wa kijinsia.
"Suala la 50 kwa 50 haliji hivi hivi wanawake wanahitaji kushikwa mkono na sisi kama ERB tumeweka mikakati kwa malengo ya kufikisha usawa huo wa kijinsia ifikapo mwaka 2030".Amesema Mhandisi Kavishe

Ameeleza kuwa ERB ina miradi mbalimbali ya kuwawezesha wasichana kusoma masomo ya Sayansi na Hisabati kwa Shule za msingi na Sekondari ujulikanao kama SSP (Stem Support Program) ambao unawezesha shule kupata walimu wa Sayansi, Maabara pamoja na Maktaba laini kwa shule hizo.

Mradi mwingine ni mradi wa kuwawezesha wanawake wahitimu wa fani ya uhandisi kuweza kusajiliwa yaani SEAP zenye upendeleo chanya kwa wasichana.

Msajili huyo pia wa ERB Mhandisi Bernard Kavishe ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwa kinara katika kumuinua mtoto wa kike hususani katika ujenzi wa shule za sekondari za Sayansi za wasichana 26 kote nchini.

ERB inatoa wito kwa jamii kuunga mkono uwekezaji wa Rais Samia kwa kuchangia walimu na vitabu laini kupitia miradi kama Stem Support Program (SSP) unaoratibiwa na bodi hiyo ya usajili wa wahandisi.

No comments:

Post a Comment