
Wananchi wa Kijiji cha Mlongia wilayani Chemba wameliomba Jeshi la Polisi mkoani Dodoma kuwajengea kituo kidogo cha polisi katika Kijiji hicho ili kudhibiti vitendo vya kihalifu vinavyofanywa na baadhi ya wananchi na kuleta taharuki.
Hayo yamejiri Februari 17,2025 wakati wa mkutano wa hadhara na wanakijiji kata ya Mlongia na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) George Katabazi alipofika kijijini hapo kuzungumza na wakazi wa eneo hilo juu ya masuala ulinzi na usalama pomoja na kusikiliza kero.
Katabazi amewahakikishia usalama wananchi hao pamoja hatua zilizochukuliwa na Jeshi la Polisi za kuwakamata watuhumiwa Saba walio kuwa wakifanya uhalifu wanaojulikana kwa kundi la Maronjoo na kuwafikisha Mahakani.
Wananchi wa eneo hilo pia wamepongeza hatua zilizo chukuliwa na kuahidi kutoa ushirikiano kwa kutoa ushahidi mahakamani ili kuweza kutokomeza uhalifu katika kijiji hicho.





No comments:
Post a Comment