MAADHIMISHO YA WIKI YA MAKAZI YATAONGEZA HAMASA YA KUTAMBUA NA KUTUMIA ANWANI ZA MAKAZI KATIKA SHUGHULI ZA KIJAMII NA KIUCHUMI - DKT. SILAA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, February 6, 2025

MAADHIMISHO YA WIKI YA MAKAZI YATAONGEZA HAMASA YA KUTAMBUA NA KUTUMIA ANWANI ZA MAKAZI KATIKA SHUGHULI ZA KIJAMII NA KIUCHUMI - DKT. SILAA.


Na Carlos Claudio, Dodoma

Wananchi wametakiwa kufahamu anwani zao za makazi na kuzitumia katika kujitambulisha ili kurahisisha utoaji na upokeaji wa huduma mbalimbali na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.


Hayo yamesemwa leo Februari 6, 2025 jijini Dodoma na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari  Mhe. Jerry William Silaa alipofungua maadhimisho ya wiki ya anwani za makazi nchini katika viwanja vya Jakaya Kikwete Convention Centre.


Amesema mfumo wa anwani za makazi ni muunganiko wa taarifa na miundombinu ambayo kwa pamoja inatambulisha anwani halisi ya kitu au mtu  alipo ili kurahisisha utoaji na upokeaji wa huduma hivyo kwa kutambua hilo serikali kupitia wizara ya mawasiliano na teknolojia ya habari kwa kushirikiana na wadau wengine hususan Ofisi ya Rais-TAMISEMI na wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi inaratibu utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi nchini.


“Dhamira ya serikali ni kuhakikisha kuwa kila nyumba, jengo, kiwanja, huduma, ofisi ama eneo la biashara linatambulika kwa anwani ya makazi, anwani ya Makazi inaundwa na namba ya anwani maarufu kama namba ya nyumba, Jina la barabara au mtaa na Postikodi,”


“Anwani za makazi inarahisisha utoaji na upokeaji wa huduma mbalimbali ili kuchochea maendeleo ya Kiuchumi na kijamii hasa katika zama hizi ambazo Mapinduzi ya 4,5 na 6 ya viwanda yanategemea matumizi ya TEHAMA.” amesema Silaa


Aidha amesema utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi ulianza mwaka 2010 na kwa mujibu wa mpango wa utekelezaji ulitakiwa ukamilike mwaka 2015 hata hivyo, utekelezaji wake ulikuwa wa kasi ndogo ukilinganisha na matarijio, hali iliyosababisha kuanzishwa kwa operesheni maalumu iliyojulikana kama operesheni anwani za makazi ambayo ilizinduliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Februari, 8, 2022.


Sambamba na hayo amesema kuwa utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi ni endelevu kwa sababu ya mabadiliko ya makazi, wakazi, na huduma hivyo shughuli mbalimbali za mfumo zinaendelea kutekelezwa ikiwemo kukusanya, kuhakiki na kuhuisha taarifa za anwani za makazi, kuboresha utendaji kazi wa Mfumo wa NaPA, kutoa elimu kwa umma na kuhamasisha utekelezaji, uendelezaji na matumizi ya mfumo wa anwani za makazi.



Kwa upande wake Naibu Waziri wa OR- TAMISEMI, Mhe. Festo Dugange akimuwakilisha Waziri Mchengerwa katika hotuba yake amesema OR- TAMISEMI ni wadau wakuu katika utekelezaji hususan kupitia kwa Watendaji wa Kata, Vijiji na Mitaa ambao wana wajibu wa kuwezesha uwekaji wa miundombinu, kuhuisha taarifa, na kukusanya taarifa mpya huku ikinufaika katika matumizi ya mfumo huo.


“Kwa upande wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na OR- TAMISEMI tumekubaliana kuendelea kutoa mafunzo ya mfumo wa anwani za makazi  kwa waratibu wa mikoa na Hhalmashauri.”


Dugange amesema  kuwa “mafunzo mengine yatakuwa yanatolewa kwa njia ya TEHAMA (online training), hivyo Makatibu Tawala wa Mikoa na wakurugenzi wa halmashauri muwaruhusu, muwahamasishe na muwahimize waratibu wenu kushiriki mafunzo haya kwa kadri ratiba zitakazoandaliwa”.


maadhimisho hayo ya kwanza kitaifa yanaongozwa na kauli mbiu ya “Tambua na tumia anwani za makazi kurahisisha utoaji na upokeaji wa hudumua“.








No comments:

Post a Comment