Na Carlos Claudio, Dodoma.
Changamoto za vipimo zimekuwa zikiongezeka mkoa wa Dodoma zinazosababishwa na muingiliano wa wafanyabiashara kutokana na miradi mikubwa inayoendelea ikiwemo mradi wa treni ya kisasa SGR unaochochea mkoa huo kuwa kitivo cha biashara.
Hayo yamesemwa na Afisa Rasilimali watu mkoa wa Dodoma Coletha Kiwale akimuwakilisha Katibu tawala wa mkoa huo katika shughuli ya futari iliyoandaliwa na Wakala wa Vipimo ikiwa na lengo la kupata dua ambayo itafungua mafanikio waliyoyapata kukamilisha ujenzi wa jengo la ofisi ya makao makuu.
Amesema changamoto za vipimo zitaemda kutatuliwa kwa ujenzi wa jengo hilo ambalo litawapa watumishi nafasi nzuri ya kufanya kazi pamoja na kuhudumia vyema wateja.
“Sisi ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma tutaendelea kushirikiana na ofisi ya wakala wa vipimo kuhakikisha kwamba changamoto za walaji ambazo zitajitokeza zitaendelea kufanyiwa kazi”,
“Na nipende kusema tu kwamba Wakala wa Vipimo wamekuwa wakiendelea kutatua changamoto za vipimo kwa walaji kwa nyakati zote, siyo kwamba walikuwa hawafanyi lakini kwa changamoto ambazo zimejitokeza tumeweza kuzitatua pamoja na zile ambazo zitajitokeza tutashirikiana nao kuzitatua”, amesema Coletha.
Nae Mjumbe wa bodi Wakala wa Vipimo CPA Swelehe Chindoma amesema Wakala wa Vipimo ina shughuli ya kusimamia vipimo vyote nchini hivyo dhamira yao ni kuhakikisha wanampatia mlaji haki yake kutokana na kipimo stahiki.
Amesema ni dhambi kubwa kupunja kipimo kwani hata vitabu vya dini (Biblia na Qur'an) vinakumbusha waumini umuhimu wa vipimo sahihi hivyo jukumu lao ni kutoa elimu ya matumizi sahihi ya vipimo kwa wananchi.
“Adhabu kubwa katika eneo hili linatolewa na mwenyezi Mungu lakini pia sheria zetu zinatoa adhabu kwa wale ambao wanapunja vipimo, sisi sote kwa pamoja tunashauriwa kutenda haki, anayepaswa kupata kilo mmoja basi apewe sawa sawa na thamani ya fedha ambayo ameilipa,” amesema …….
Kwa upande wake msemaji wa shekh wa mkoa wa Dodoma Sheikh Ahmad Said akimuwakilisha shekh wa Mkoa amesema ofisi hiyo inafanya kazi ya kurekebisha tabia ya baadhi ya watu wenye nia ya kuwadhulumu wengine kwa njia ya vipimo
Sheikh Said ameongeza na kusema,“ naipongeza sana ofisi hii pamoja na wote mliopo katika ofisi hii, endeleeni kufanya kazi hii kwasababu ni kazi kubwa ya kurekebisha tabia ya watu wanaodhulumu”.
No comments:
Post a Comment