
Wazee wa Yanga mkoa wa Dodoma wamecharuka na kutoa Saa 72 kwa Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia kuomba radhi kufuatilia kauli aliyoitoa kuhusu timu yao.
Kauli hiyo imetolewa leo Machi 18,2025 jijini Dodoma mbele ya Waandishi wa habari na Mzee Abdalah Mtosa kwa niaba ya wazee wengine huku akisisitiza hawaoni sababu ya kurudia mchezo ambao tayari ulipangwa kisheria na kuahirishwa bila utaratibu siku ya Machi 8,2025
Mzee Mtosa amesema siku pekee ambayo ilikuwa halali kwa mchezo huo kuchezwa tayari imepita na ilikuwa inatosha kabisa kuwakutanisha watani kwani maandalizi yote yalikuwa yameshakamilika.
"Nimepokea kwa masikitiko makubwa sana Kwa kuahirishwa kwa mchezo wa Machi 8 mwaka huu, kwahiyo na sisi hatuna imani na karia kwani tunajua wazi hana mapenzi ya dhati na yanga
hivyo niwaombe viongozi wa juu kutokuruhusu mechi kufanyika tena Kwa wakati mwingine kama ni faini tuko tayari kulipa lakini sio kurudia mechi na simba". amesema Mtosa
Naye Mzee Bodar Awadhi amesema mechi kuahirishwa imefanya kutokea mkanganyiko na sintofahamu kwa mashabiki wa soka na hivyo kundi kubwa halitaki tena hiyo mechi.
Kauli ya kutokuwa na imani tena na Rais Karia imekuja mara baada ya kuahirishwa Kwa dabi ya karikakoo na Kutokana na kauli aliyoitoa ambayo wameita kauli ya kuwafokea.
"Sisi msimamo wetu ni kutokurudia mechi kwanza RAIS wa TFF ametudhalilisha wanayanga na kama ameshindwa mpira arudi kwenye taaluma yake kwani tunaijua"
Kwa upande wake Mratibu wa yanga Dodoma Elisha Ngwando amesema Karia aombe Radhi kwa Wanachama wa Yanga na wanamichezo kwa alichokifanya na kauli aliyoitoa.
"Watu wametumia gharama kubwa wengine wamelipia matangazo kwa ajili ya mechi hiyo"





No comments:
Post a Comment