KAMATI YA BUNGE YA PAC YAIPONGEZA TANROADS KWA KASI UJENZI BARABARA YA MZUNGUKO WA NJE YA JIJI LA DODOMA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, April 5, 2025

KAMATI YA BUNGE YA PAC YAIPONGEZA TANROADS KWA KASI UJENZI BARABARA YA MZUNGUKO WA NJE YA JIJI LA DODOMA.

 


Na Carlos Claudio, Dodoma.


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeipongeza Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), kwa utekelezaji mzuri wa ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara ya mzunguko wa nje ya jiji la Dodoma ambapo utekelezaji wake umefikia takribani asilimia 84.72 ukilinganisha na asilimia 82.19 za mpango kazi wa Mkandarasi.  


Pongezi hizo zimetolewa leo Aprili 3,2025 na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Naghenjwa Kaboyoka mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa KM 112.3 huku ikiitaka Wizara kumsimamia Mkandarasi ili kuhakikisha muda uliosalia anakamilisha ujenzi.





"Niwashukuru sana, niwashukuru wote ambao mmehusika katika kazi hii pamoja na CAG kwa kuangalia na kuona fedha ya umma imetumika vizuri, pamoja na shukrani kwa waheshimiwa wabunge maana mmeshuhudia wenyewe na mmetoa pongezi hizi na kwa kweli kazi ni nzuri,”


"Leo tumeshuhudia ujenzi wa barabara unaendelea vizuri na hiko katika viwango vizuri sana hivyo kamati yetu imeridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa barabara  hii na tumeipongeza Wizara kwa kusimamia vizuri pamoja na mkandarasi na mshauri mwelekezi kwa kufanya kazi vizuri, "amesema. 



Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania( TANROADS) Mha. Mohamedi Besta amesema kuwa TANROADS pamoja na TRC wanashirikiana kwa karibu kuhakikisha wanatekeleza na kukamilisha daraja ambalo ni mapishano ya reli pamoja na barabara.



“Wizara yetu kwa kupitia makatibu wakuu wetu pamoja na wataalam kati yetu sisi TANROADS kwa upande mmoja lakini na TRC tumekuwa tukifanya kazi kwa karibu sana, ujenzi wa barabara unaenda kwa kasi lakini kwenye eneo hili nyuma yangu ndio ambapo wenzetu wa TRC kwa muujibu wa ujenzi walianza kuchimba ili kujenga hilo daraja, kwaio nilikuwa natoa taarifa hiyo ya msingi ili kujua eneo moja wapo ambalo wenzetu wa TRC wanatakiwa wajenge kupishanisha,”amesema.



Naye Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Janeth Masaburi ametoa pongezi kwa  Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza kikamilifu na uaminifu miradi iliyoacha na serikali ya awamu ya tano huku akiitaka TANROADS kuzingatia alama za barabara hiyo mara baada ya ujenzi kukamilika.


“niipongeze Wizara kwa usimamizi, niipongeze TANROADS, wakandarasi na watendaji wote kwa kazi njema iliyofanyika, wafanyakazi 378 wamenufaika huku watanzania wakiwa 355 sawa na asilimia 93.9 tunashukuru sana na hii ndio tunataka ili kuwawezesha wananchi wetu waweze kupata ajira kutokana na miradi,” amesema Janeth.


Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Dkt. Charles Msonde, ameeleza changamoto zinazowakabili ikiwa ni ujenzi wa madaraja mawili ya mapishano ya reli ya SGR pamoja na barabara huku mradi huo wa ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje ya jiji la Dodoma ukitarajia kukamilika Agasti 31, 2025.












No comments:

Post a Comment