DKT. YONAZI AFIKA MSIBANI KWA HAYATI MSUYA, ATOA SALAMU ZA POLE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, May 8, 2025

DKT. YONAZI AFIKA MSIBANI KWA HAYATI MSUYA, ATOA SALAMU ZA POLE



NA. MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amefika msibani kwa Hayati Cleopa Msuya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye aliyefariki tarehe 07 Mei, 2025 katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.

Dkt. Yonazi amefika nyumbani kwa hayati Cleopa Msuya Upanga Jijijni Dar es Salaam akiongozana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ally Senga Gugu na kutoa salamu za pole kwa familia ya Hayati Msuya.


No comments:

Post a Comment